Sunday, July 15, 2012

MH MKONO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA SEKONDARI YA BUTUGURI
         Madawati yaliyotengenezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ambayo Mh Mkono amesema hayafai kutumika
                 Mh Mkono akiangalia madawati yaliyotengenezwa na TASAF
                   Mh Mkono na George Marato wakiteta Jambo
                     Shule ya sekondary Butuguri inavyoonekana
                    Diwani wa Nyegine Thomas Nyasiro
             Diwani Bukima  Luta Mayamba
                      Mandhari ya shule hiyo sakafuni
                   Marekebisho yanendelea
                                   Muonekano ulivyo katika sekondary ya Butuguri
                                  Ukaguzi unaendelea
                       Matengenezo yanaendelea katika shule ya sekondary Butuguri
       Mwakilishi wa ITV & Redio one George Marato akiongozana na Mh Mkono  katika ukaguzi wa kushtukiza katika sekondary ya Butuguri wilayani Butiama

 
MUSOMA

Madawati zaidi ya 1000 yaliyotengenezwa na Mfuko wa  Maendeleo  ya Jamii TASAF, kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Butuguri iliyopo katika Halmshauri ya Musoma mkoani Mara yamebainika kuwa hayafai kwa matumizi shuleni hapo.

Akiongea na waandishi wa habari Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono amesema kuwa kumekuwepo na wizi mkubwa katika miradi mbalimbali ya TASAF hivyo hayuko tayari kuona wizi huo unaendelea katika jimbo hilo

Amesema  miradi iliyotengenezwa na Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii haifai ikilinganishwa na shule hiyo ya Butuguri aliyoijenga kwa fedha zake,huku wezi wa fedha za mfuko huo wakiendelea kulindwa
Mh Mkono amesema kuwa kumekuwepo na desturi ya kumkamata mwizi wa kuku na kumua lakini watu wanaoiba na kutumia fedha za Umma vibaya wakiachwa bila kukamatwa.

Mbunge huyo akionyesha kukasirika kutokana na ubadhilifu huo wa fedha za Madawati hayo amesema atabeba madawati hayo na kuyarudisha katika halmashauri hiyo na yeye kuleta madawati mengine kwa matumizi shuleni hapo

Aidha madiwani kutoka Halmashauri hiyo Luti Mayamba na Thomas Nyasiro waliokuwa wameambatana na Mbunge huyo wamesema vitendo hivyo si vya kiungwana kwani inaonyesha dhahiri viongozi wanavyotumia madaraka yao vibaya na kuahidi kufika suala hilo katika baraza la madiwani ili hatua stahiki zichukuliwe.

Madawati hayo zaidi ya 1000 yaliyotengenzwa na MfuKo wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa zaidi ya shilingi milioni 50 chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashuri hiyo Dr Karnai Kunei yameharibika muda mfupi mara baada ya kuanza kutumika

No comments:

Post a Comment