MKONO KUUNGANISHA TARAFA YA NYANJA NA MAKONGORO
Wakulima wa tarafa za Makongoro na Nyanja, katika wilaya ya Butiama Mkoani
Mara pamoja na baadhi ya vijiji vya wilaya ya Bunda,wataanza kunufaika na masoko
ya mazao yao baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara inayojengwa na mbunge
wa jimbo la Musoma vijijini Nimrod Mkono.
Barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha changarawe inatarajia kugharamu zaidi
ya shilingi milioni 80 ambapo ikikamilika italeta msaada mkubwa kwa wakulima
kuweza kupata soko la uhakika la mazao yao.
Barabara inayojengwa na Mh Nimroad Mkono,Mbunge wa jimbo la Musoma (v)
Kwa miaka mingi wakulima wa maeneo hayo wamekuwa wakilazimika kuuza mazao yao yakiwa bado mashambani kutokana na ukosefu wa miundombinu ya barabara na hivyo kupelekea kuuza mazao hayo katika bei isiyoridhisha na inayowaumiza wakulima hao
Akiongea baada ya ukaguzi wa barabara hiyo mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono, amesema kilichomsukuma kufikia uamuzi wa kujenga barabara hiyo kwa fedha zake ni kutokana na wananchi wa eneo hilo kupata taabu ya kuuza mazao yao na kwa bei isiyoridhisha
Baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo, wamesema tatizo la ukosefu wa barabara limekuwa ni kikwazo kikubwa wakati wanapohitaji kuuza mazao yao sokoni, pia limekuwa likisababisha baadhi ya akina mama wajawazito na watoto kushindwa kufika kwa wakati katika zahanati na vituo vya afya.
Hadi sasa, mbunge Nimrod Mkono ameweza kujenga barabara zaidi ya tano katika wilaya ya Butiama kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 400, jambo ambalo limerahisisha mawasiliano katika maeneo mbalimbali, huku halmashauri ya wilaya ya Musoma ikitumia barabara hizo kama miradi yake inayoitekeleza

No comments:
Post a Comment