MWENYEKITI CHAMA CHA SOKA MARA AFARIKI DUNIA
Na Shomari Binda
Musoma
Chama cha soka mkoani Mara, FAM kimepata pigo kubwa kufuatia
kifo cha mwenyekiti wake Fabian Samo, kilichotokea jumanne asubuhi
katika hospitali ya mkoa wa Mara mjini Musoma.
Samo ambaye alichaguliwa kushika wadhifa huo, kwa mara ya pili
mfululizo katika uchaguzi mkuu uliofanyikia Shirati, wilayani Rorya
Novemba 13 mwaka jana baada ya kumshinda mpinzani wake Sospeter Masambu,
ameelezwa na baadhi ya wadau wa soka wa mikoa ya Mwanza na Mara kwamba
alikuwa ni nguzo na mhimili mkubwa katika kuendeleza fani ya mchezo wa
soka.
Katibu wa Chama cha Soka mkoa wa Mara Mugisha Galibona, amesema
marehemu Fabian Samo atakumbukwa kwa mengi, ikiwemo msimamo wake katika
maamuzi na makubaliano na zaidi alikuwa mstari wa mbele katika
kuhakikisha kiwango cha soka mkoani Mara kinapanda.
Galibona pia amedai marehemu Samo, alikuwa ni kiungo muhimu baina ya
viongozi wa juu wa shirikisho la soka nchini TFF, na wadau mbalimbali
wa soka hasa pale timu za mkoa huu zilipokuwa zikisafiri nje ya mkoa
katika mashindano ya kombe la taifa na mashindano ya vijana chini ya
miaka 17, ya Copa Coca Cola.
Kwa upande wake, mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF anayesimamia
masuala ya soka katika mikoa ya Mwanza na Mara, Samwel Nyalla
akizungumza na Mwandishi wa BROGU hii kwa njia ya simu kutoka Mwanza
amesema, amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha kiongozi huyo kwani
alikuwa bado akihitajika kwa mawazo na michango yake mbalimbali katika
kuendeleza mchezo wa soka.
Aidha, mjumbe wa kamati ya soka la vijana na wanawake mkoa wa Mara
Shomari Binda, akielezea mchango wa marehemu Samo katika medani ya
soka, amesema kiongozi huyo ataendelea kukumbwa daima kwa jinsi
alivyosimamia maendeleo ya soka la vijana na wanawake kwa kutoa miongozo
mbalimbali katika kutaka kufanikisha.
Binda amesema kabla ya kufikwa na mauti marehemu fabian Samo licha ya kuwa katika maradhi alikuwa akifatilia maendeleo ya timu ya vijana ya mkoa wa Mara iliyo na umri chini ya miaka 17 iliyokuwa jijini Dar es salaam kwa ajili ya ushiriki wa mashindano ya Copa Coca Cola ambayo ilitolewa katika hatua ya robo fainali na vijana wenzao wa Mkoa wa Morogoro.
Naye mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Musoma mjini, aliye pia
mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF David Sungura amesema kifo cha marehemu
Fabian Samo kimekuja wakati timu ya Polisi Mara ikiwa bado inahitaji
mchango wake wa mawazo katika maandalizi ya michezo ya ligi daraja la
kwanza iliyopata nafasi hiyo hivi karibuni..
Marehemu Fabian Samo atazikwa siku ya ijumaa saa saba mchana nyumbani kwake katika kata ya Nyakato Manispaa ya Musoma baada ya shughuli za ibada na wadau wa soka kutoa heshima zao za mwis

No comments:
Post a Comment