WAUOMBA MGODI WA NORTH MARA
KUWAHAMISHA.
Dinna Maningo,Tarime. (Mwana wa Afrika blogsport.com)
WANANCHI wa Kitongoji cha
Nyabichune Kijiji ch nyangoto-Nyamongo Wilayani Tarime wanaoishi jirani na
Mgodi wameuomba Mgodi huo wa Dhahabu wa North Mara kuwahamisha kwa madai kuwa maeneo wanayoishi ni maeneo
hatarishi kwa maisha yao.
Walisema kuwa kutokana na
shughuli za Mgodi na Mgodi huo kuwa jirani na makazi ya watu umekuwa ni kero
kwao na hivyo kusababisha wananchi
kuishi kwa hofu kwa kuofia usalama wao.
Kuomba kuhamishwa kwa
wananchi wa kitongoji cha Nyabichune
kumekuja baada ya kudaiwa kuporomoka mawe kutoka mgodini mara kwa mara hadi kwenye nyumba za watu na kwamba siku
chache zilizopita kuna jiwe kubwa liliporomoka na kubomoa sehemu ya nyumba ya Juma
magabe anayeishi jirani na Mgodi huo.
“Mgodi unilipe fidia na
kibidi utuhamishe maeneo tunayoishi ni hatarishi kutoka nyumbani kwangu
ninakoishi ni hatua 5 hadi mgodini,kuna mawe yaliyoifadhiwa na yako mgodini
ambayo hayana dhahabu yamekuwa yakipolomoka hadi kwenye nyumba zetu hivi karibuni
majira ya saa 10 jioni liliporomoka jiwe kubwa likabomoa sehemu ya nymba ya
mama yangu”alisema Juma magabe.
Aliongeza”ni hatari kwa
maisha yetu kuna watoto ucheza kiasi kwamba ipo siku litamporomokea na
kumuuwa hali hiyo imesababisha mama
ameogopa kuishi kwenye hiyo nyumba nimejaribu kufatilia Serikali ya kijiji
Mtendaji akaniandikia barua ya malalamiko nikaipeleka mgodini lakini hadi sasa
hakuna jitihada zozote zilizofanyika nia yangu naomba Mgodi unifanyie tathimini
unilipe mimi na familia yangu tuhame”aliasema Magabe.
Mtendaji wa Kjiji cha
Nyangoto Samwel Philipo alikiri kuwepo kwa tatizo la kuporomoka kwa mawe kwenye
makazi ya watu na kuthibitisha kubomoka kwa Nyumba ya mkazi mmoja baada ya
kudondokewa na jiwe nakwamba tayali alishawasiliana na mgodi ili kutatua tatizo
hilo ikiwa ni pamoja na kuutaka
mgodi kuwahamisha watu wote waishio
maeneo hatarishi jirani na Mgodi.
Ghati Marwa mkazi wa
kitongoji cha Nyabichune alisema kuwa mbali na kuporomoka kwa mawe pia shughuri
za mgodi zimekuwa ni kero kwao hususani baruti zenye milio mikali na mitikisiko
mikubwa zinazopigwa kutoka ndani na mgodi pamoja na mabomu ya machozi
yanayopigwa hewani na Askari wanaolinda mgodi na kusababisha kusambaa kwa moshi
unaoathiri afya zao.
Hata hivyo uongozi wa Mgodi
wa North Mara ulikiri kuporomoka kwa mawe kwenye makazi ya watu ambapo walikiri
kubomoka kwa nyumba baada ya kuangukiwa na jiwe kubwa lililotoka Mgodini ambapo
walisema kuwa wanafanya utaratibu ili
kufanya tathimini kwa wakazi wa Kitongoji cha Nyabichune waishio maeneo
hatarishi jirani na Mgodi ambapo tathimini hiyo itaambatana na malipo na kisha
kuyahama makazi hayo yaliyo jirani na Mgodi.
No comments:
Post a Comment