VIONGOZI WANNE WA UAMSHO ZANZIBAR WAJISALIMISHA POLISI
Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi- Zanzibar
VIONGOZI wanne wa Kundi la Uamsho waliohusika katika uchochezi wa
vurugu za wiki iliyopita mjini zanzibar, leo wamejisalimisha kwa
Makachero wa Jeshi la Polisi na kuhojiwa kwa masaa kadha kabla ya
kuachiwa kwa mashariti.
Taarifa ya Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, imewataja viongozi waliojisalimisha kuwa ni Shekhe Suleiman Juma(62) mkazi wa Makadara na Shekhe Fikirini Majaliwa(47), mkazi wa Jang’ombe.
Taarifa
hiyo imewataja wengine waliojisalimisha kuwa ni pamoja na Katibu wa
Jumuia ya Uamsho Sheikhe Abdallah Saidi(45), mkazi wa Misufini pamoja na
Afisa Usalama wa Jumuiya hiyo Bw. Haji Sadifa(51), mkazi wa
Mwembenjugu.
Viongozi
hao pamoja na mpambe wao, walijisalimisha mapema asubuhi leo kwa
Viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Mangaribi Zanzibar na kuhojiwa
kwa muda kabla ya kupelekwa Makao Makuu ya Upelelezi Zanzibar kwa mahojiano zaidi na baadaye kuachiliwa kwa dhamana.
Tangu
kutokea kwa vurugu zilizopelekea kukamatwa kwa baadhi ya wafuasi wa
kundi la Uamsho mjini Zanzbar na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zao, viongozi hao watatu pamoja na mpambe wao walikuwa hawajapatikana.
Mara
baada ya vurugu hizo za wiki iliyopita, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP
Mussa Ali Mussa, alisema kuwa Jeshi la Polisi litahakikisha kuwa wale
wote waliochoche vurugu hizo wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu
mashtaka yao.
Katika
vurugu hizo zilizodumu kwa muda wa siku tatu, pia zilizopelekea
kuchomwa moto kwa baadhi ya makanisa na mali nyingine za madukani
kuporwa na nyingine kuharibiwa na wafuasi wa kikundi hicho.
Jeshi
la Polisi Visiwani hapa limeendelea kutoa wito kwa viongozi wengine
walioshiriki katika vurugu hizo kujisalimisha wenye Polisi badala ya
kusubiri kutafutwa.
Hadi
sasa watuhumiwa 78 wakiwemo viongozi wa kundi la Uamsho, wamekamatwa na
kufikishwa mahakamani ambapo baadhi yao wameachiliwa kwa dhamana na
wengine wakipelekwa rumande kwa kukosa wadhamini wenye kuaminika hadi
Juni 11, mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment