VIONGOZI WENGINE WAWILI WA UAMSHO ZANZIBAR WAJISALIMISHA POLISI
Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi, Zanzibar
VIONGOZI wengine wawili wa Jumuiya ya Uamsho Visiwani Zanzibar, leo
wamefika Makao Makuu ya Upelelezi Zanzibar ambako walihojiwa kwa muda
kuhusiana na vurugu za wiki iliyopita visiwani hapa kabla ya kuachiliwa.
Afisa
Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina,
amewataja Viongozi waliofika Polisi na kuhojiwa kuwa ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Uamshio Shekhe Mselem Bin Ali, mkazi wa Makadara na Shekhe
Azan Ahmed Saidi, wa Mfenesini.
Inspekta
Mhina amesema katika mahojiano hayo Polisi walibaini kuwa siku ya
vurugu hizo, viongozi hao hawakuwepo mjini Zanzibar ingawa Polisi
walitaka kujua zaidi kama wao walihusika katika maandalizi ya awali ya
mpango huo kabla ya kuondoka kisiwani hapa.
Wakati
wa matukio hayo Sheikhe Mselem alikuwa Pemba na Shekhe Azan alikuwa
Uwarabuni kwa matibabu lakini alilazimika kurejea Zanzibar baada ya
kusikia hali ya vurugu zilizofanywa na vijana wa kikundi chake.
Viongozi
hao wanafanya idadi ya viongozi waandamizi wa Jumuiya hiyo
waliojisalimisha na kuhojiwa kwa hiyari na Makachero wa Jeshi la Polisi
mjini Zanzibar kufikia sita.
Jana
viongozi wengine wanne kutoka katika kundi hilo la Uamsho,
walijisalimisha wenyewe Polisi na kuhojiwa kwa masaa kadhaa kabla ya
kuachiwa kwa masharti.
Inspekta
Mhina amesema kuwa bado Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa
viongozi wengine wa Jumuiya hiyo ambao hawajafika Polisi, kufanya hivyo
badala ya kusakwa na kutiwa nguvuni kuhusiana na vurugu hizo.
Wiki
iliyopita Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Emmanuel Nchimbi na Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, walifika mjini
Zanzibar na kuwataka wale wote waliohusika katika vurugu hizo kujitokeza
kukabili mkono wa sheria.
Tayari
watu 78 wamekamatwa na Polisi na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za
kufanya vurugu zilizosababisha kuchomwa moto kwa magari na baadhi ya
makanisa mjini Zanzibar.
Mwisho
No comments:
Post a Comment