Wednesday, June 6, 2012

                             WARSHA ILIYOANDALIWA NA UMABU JUU YA HAKI ZA WATOTO

MUSOMA

JAMII IMETAKIWA KUZIELEWA NA KUZITHAMINI HAKI ZA WATOTO IKIWA NI LENGO LA KUMWEZESHA MTOTO KATIKA KUFANIKISHA MALENGO YA MILLENIA KWA MWAKA 2015
HAYO YAMESEMWA LEO NA AFISA MAENDELEO YA JAMII MANISPAA YA MUSOMA BI JANETH MAFIPA KATIKA WARSHA JUU YA HAKI ZAW WATOTO INAYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA DAYOSISI YA  ANGLIKANA MJINI MUSOMA.


AMESEMA NI JUKUMU LA JAMII KATIKA KUWAPA WATOTO HAKI ZAO ZA MSINGI AMBAZO ZIMEAINISHWA SEHEMU MBALIMBALI IKIWA NI LENGO LA KUIANDAA JAMII YENYE MAADILI.
BI. JANETH AMESEMA JAMII HAIWEZI KUENDELEA KAMA ITAPUUZA HAKI ZA WATOTO HIVYO NI VYEMA JAMII NA TAASISI MBALIMBALI ZA SERIKALI NA WATU BINAFSI WAKAZIHESHIMU HAKI ZA WATOTO .


KATIKA WARSHA HIYO AMBAYO IMEWAKUTANISHA WATU MBALIMBALI KUTOKA MKOANI MARA IMELENGA KUIKUMBUSHA JAMII JUU YA KUHESHIMU NA KUZILINDA HAKI ZA WATOTO KAMA NJIA YA KUZITAMBUA SHERIA MBALIMBALI ZA KIMATAIFA AMBAZO NCHI IMERIDHIA
AIDHA MRATIBU WA  SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA  UMOJA WA  MAENDELEO YA BUKWAYA LA (UMABU) BULUDE NDAGO AMESEMA KUWA SHIRIKA HILO KWASASA LIMEJIDHATITI KATIKA KUELIMISHA MTOTO WA KIKE,KUJENGA SHULE  ZA WALIMU,UJENZI WA VYOO BORA VIJIJINI PAMOJA NA KUHIMIZA  SUALA ZIMA LA MZINGIRA


AMESEMA WARSHA HIYO YA SIKU TATU IMEANDALIWA  NA UMABU AMBALO LINAFADHILIWA NA SHIRIKA LA TERRE-DES HOMMES KUTOKA NCHINI UHOLANZI LINAJISHUGHULISHA KATIKA MASUALA YA ELIMU,MAJI NA AFYA KATIKA VIJIJI 15 MKOANI MARA
MBALI NA HIVYO PIA UMABU  INAJISHUGHULISHA NA SHUGHULI ZA UZALISHAJI MALI,UTUNZAJI WA MAZINGIRA,MASUALA YA VVU/UKIMWI  KATIKA ENEO LA BUKWAYA HALMASHAURI YA MUSOMA MKOANI MARA

No comments:

Post a Comment