POLISI KIGOMA WAPAMBANA NA MAJAMBAZI NA KUFANIKIWA KUMUUA MMOJA NA KUPATA SILAHA AINA YA SMG YENYE RISASI NNE
Na Mohammed Mhina na Pardon Mbwate, wa Jeshi la Polisi
KIGOMA JUMATANO JUNI 12, 2012 Makachero
wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma jana walilazimika kutumia risasi
kupambana na kundi la majambazi wenye silaha waliokuwa wamepanga
kumvamia mmoja wa wafanya biashara mkoani humo.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kigoma ACP. Frasser Kashai, amesema kuwa katika tukio
hilo Polisi walimpiga risasi mmoja wa majambazi hayo aliejulikana kwa
jina la Lowasi Moria(22) mkazi wa Kijiji cha Kabale mkoani humo.
Kamanda
Kashai amesema wakati wa mapambano hayo, majambazi wengine watatu
walifanikiwa kutoroka huku wakimuacha mwenzao aliyekuwa na silaha hiyo
aina ya SMG akiwa anagaragara chini kutokana na majeraha ya risasi.
Hata
hivyo Kamanda Kashai amesema jambazi huyo aliyekuwa na SMG yenye namba
TU 8453 ikiwa na risasi nne zilizobaki kwenye magazine yake alifariki
dunia wakati Polisi walipokuwa wakimpeleka Hospitali kwa matibabu.
Kamanda
kashai amesema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 06.00 mchana
huko kwenye pori la Ruhuru lililopo karibu ya kijiji cha Gwarama wilaya
ya Kibondo mkoani Kigoma.
Amesema
Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna majambazi yenye
silaha na wamepanga kuwavamia wafanyabiashara wanaopita katika eneo
hilo na ndipo askari waliokuwa wakifanya doria katika barabara hiyo
walipoamua kuweka mtego katika eneo hilo.
Kamanda
huyo amesema kuwa, wakati wakiwa katika eneo hilo, Polisi walimuona mtu
mmoja akiwa na pikipiki akitokea Kakonko kwenda Muhange Kabale na baada
ya muda si mrefu majambazi hayo walijitokeza na kumvamia na ndipo
walipoanza kurushiana risasi na kufanikiwa kumjeruhi mmoja wao.
Katika
tukio lingine Kamanda Kashai amesema juzi majira ya saa nne usiku huko
kwenye eneo la Mwanga mjini Kigoma, dereva mmoja wa bodaboda aitwaye
Puldence Gasto(28), mkazi wa Majengo alimwagiwa tindikali usoni na
abiria aliyembeba kisha kumpora pikipiki yake.
Kamanda huyo ameitaja pikipiki iliyoporwa kuwa ni yenye namba T 692 BLZ aina ya SUNLG, rangi nyekundu ambayo hadi sasa haijajulikana mahali ilipo.
Amesema
dereva huyo wa bodaboda amelazwa kwenye hospitali ya mkoa ya Maweni kwa
matibabu zaidi wakati Polisi wakiendelea na msako dhidi mtuhumiwa
pamoja na pikipiki hiyo.
Kufuatia
tukio hilo, Kamanda Kashai, ametoa wito kwa vijana waendesha boda boda
mkoani humo, kuwa na ushirikiano na kwamba kila mmoja wao amzingatie
abiria aliyechukuliwa na mmoja wao ili iwe rahisi kumkamata linapotokea
tatizo kama hilo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment