MTOTO MCHANGA AOKOTWA HAI AKIWA AMETUPWA KWENYE
MIBA.
Dinna Maningo,Tarime
Mganga mfawidhi wa Hospitali
ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Marco Nega amewataka wanawake kuepukana
na mimba ambao hazijatarajiwa ili kuepukana na tatizo linaloendelea
nchini la kutupwa kwa watoto wachanga pindi wanapozaliwa.
Akiongea
na waandishi wa habari ofisini kwake Nega alisema kuwa imefika wakati
wanawake watambue umuhimu na haki ya mtoto ya kuishi kwani wanawake
wamekuwa wakibeba ujauzito na kisha kutoa mimba huku wanawake wengine
wakitupa watoto wachanga pindi wanapojifungua.
Dactari Nega
alisema kuwa mnamo tarehe 10 siku ya jumapili asubuhi mtoto mchanga
akiwa ameokotwa na msamalia mwema akiwa ametupwa kwenye fensi ya miba
mtaa wa Bomani mjini Tarime alifikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya
matibabu baada ya kuonekana mwili
wake kuchomwa na miba.
"Wanawake wamepukane na mimba
zisizotarajiwa hii itasaidia kupunguza tatizo la watoto wachanga kutupwa
au kunyongwa pindi wazaliwapo,ikishindikana wafuate uzazi wa mpango
hospitali inatoa huduma bure na siyo kutupa mtoto ambaye umemlea kwa
miezi 9 tumboni leo hii mama anajifungua na kutupa mtoto huo ni ukatiki
kwa mtoto asiye na hatia"alisema Nega.
"Anaongeza"tumempokea
mtoto kutoka kwa msamalia mwema tunampatia matibabu kwa sababu alikuwa
amechomwa na miba tumeitoa miba yote na kumpaka dawa na sasa anaendelea
vizuri anapatiwa uduma ya kunyweshwa maziwa wa ng'ombena mama
aliyemwokota ndiye anaye hapa hospitalini anamlea wakati tunafanya
maandalizi ya kumpeleka kituo cha Misheni cha kulelea watoto kilichopo
Nyabange Musoma, Serikali haina vituo vya kutunza watoto kama hao
wakifika hospitalini tunaomba kituo cha misheni wakikubali tunawapelekea
ili wawalee.
Hellena Bon alisema kuwa alimwokota mtoto
huyo aliyekuwa ametupwa katika fensi ya miba Nyumani kwakwe nakwamba
yuko tayali kumlea mtoto huyo baada ya kutimiza miaka 2 atakayolelewa
kwenye kituo cha misheni Musoma.
"Tunahisi mtoto alitupwa usiku
wa saa 6 siku ya jumamosi usiku huo tulisikia sauti ya mtoto akilia
nilifikili ni kwa jilani tukalala ilipofika jumapili asubuhi mwanangu
akiwa anafagia uwanja alimkuta mtoto huyo akiwa ametupwa kwenye fensi ya
miba ikabidi tuchukue panga na kukatakata ili kumfikia mtoto bahati
nzuri alikuwa hai mtoto wa kiume isipokuwa alikuwa amechomwa na miba
katika sehemu za mwili nikampeleka hospitali nashukuru amepatiwa huduma
nzuri na anaendelea vizuri kama unavyomuona anakunywa maziwa ya Ng'ombe
na sasa anafanyiwa utaratibu apelekwe kituo cha kulelea watoto
atakapofikisha miaka 2 ntamchukua na kumtunza ntakuwa namtembelea
tumempatia jina la baraka kwa sababu ni muujiza wa mungu maana mtoto
kakesha kwenye baridi tena akiwa uchi wa myama akiwa
ameochoma miba na wakati huo kitovu kilikuwa wazi lakini yuko hai hadi
sasa hata tulipomwokota hakuwa na mduu yeyote."alisema mama huyo.
Pia
mganga Nega ameishauri Serikali kuanzisha vituo vya kulelea watoto
katika hospitali za Wilaya na Mkoa kama njia ya kurahisisha uduma kwa
watoto kama hao na kuongeza kuwa kuna haja ya elimu ya uzazi
kufundishwa mashuleni ili wanafunzi waelewe jinsi ya kujikinga na
kuondokana na mimba zisizotarajiwa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa
kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha alisibitisha kuokotwa kwa
kichanga hicho na kwamba hadi sasa hakuna aliyekamatwa kutupa mtoto huyo
ambapo pia amewataka wananchi kwa kushirikiana na polisi kumbaini
muhusika wa tukio hilo la kutupa mtoto.
No comments:
Post a Comment