PIKIPIKI YAGONGA NA KUUA, DEREVA WA BODABODA AVUNJIKA TAYA
Na Mohammed Mhina na Pardon Mbwate, wa Jeshi la Polisi
KIGOMA ALHAMISI JUNI 14, 2012 Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa kijiji cha Muhunga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Vesta Mahwa, amefariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki huko kwenye Barabara ya Lumumba eneo la Mwanga mjini Kigoma.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kigoma ACP. Frasser Kashai, amesema kuwa ajali hiyo
ilimetokea majira ya saa 12.45 jioni ya Jumapili wiki iliyopita huko kwenye Barabara ya Lumumba Mwanga mjini Kigoma.
Amesema
ajali hiyo ilitokea wakati Dereva mmoja wa bodaboda aitwaye Kayuza
Mgambo(35), mkazi wa Burega mkoani Kigoma alipokuwa akiende pikipiki
yake kwa mwende wa kasi na hatimaye kumgonga mzee huyo aliyekuwa akitembea pembeni mwa barabara.
Alisema
mpitanjia huyo ambaye kwa sasa ni marehemu, alipata jelaha kubwa
kichwani huku Dereva huyo wa pikipiki yeye akivunjika taya zote na
kupelekea kupoteza fahamu.
Kamanda
Kashai amesema mara baada ya ajali hiyo, majeruhi wote walichukuliwa
kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni kwa matibabu zaidi
lakini wakati madaktari walipokuwa wakiendelea kuwatibu majeruhi hao,
mzee Mahwa alifariki dunia.
Hata
hivyo, Kamanda Kashai amesema, dereva wa pikipiki ambaye alikuwa
akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa ya Maweni, hivi
sasa amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza kwa
matibabu zaidi ya taya zake.
Katika tukio lingine, Jeshi
la Polisi mkoani linamshikilia mkazi mmoja mkazi wa Mpeta Sarah
Dasse(23), kwa tuhuma za kumua mtoto wake aitwaye Zainabu Sita mwenye
umri wa mwaka mmoja na nusu kwa kumkaba shingo hadi kufa.
Kamanda
Kashai amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa chanzo cha
mauaji hayo na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka lake la
mauaji ya kikatili.
Aidha Kamanda Kashai, ametoa wito kwa madereva wa pikipiki (bodaboda) kuwa mbali
ya kujiepusha na uporwaji wa pikipiki zao na wateja, lakini pia
amewataka kuwa waangalifu barabarani ili wasiwe kikwazo ama kusababisha
ajali kwa watumiaji wengine wa barabara.
Kuhusiana
na masuala mengine ya Kiusalama, Kamanda Kashai pia amewaomba wananchi
kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za siri Polisi
endap[o watabaini kuwepo kwa uhalifu na wahalifu ili wahusika wawekewe
mitege na kutiwa mbaroni.
Mwisho
No comments:
Post a Comment