WANANCHI IKOMA WAMUHITAJI WAZIRI WA ARDHI.
Dinna Maningo,Rorya.
Wananchi wa Kijiji cha Ikoma
Kata ya Ikoma Wilayani Rorya Mkoani Mara wamemuomba Waziri wa Ardhi kufika
Kijijini hapo kutatua tatizo linaloendelea la mgogoro wa umiliki wa ardhi kwa
madai kuwa uongozi wa Mkoa wa Mara
umeshindwa kutatua tatizo la kuporywa na
kukodishwa ardhi kwa wageni kutoka Kenya na wananchi wa Kijiji cha
Nyamuhunda-Tarime.
Walisema kuwa tatizo la
wageni kukodishwa ardhi na kumilikishwa ardhi kinyume cha sheria na wale wa
kijiji cha Nyamuhunda-Tarime,ni kuendelea kuibua migogoro baina ya wanakijiji
cha Ikoma na kijiji cha Nyamuhunda.
Hayo yalibainika kwenye
mkutano wa wananchi wa kijiji cha Ikoma uliohitishwa na Mwenyekiti wa kijiji
hicho Adriano Jalando uliohudhuriwa na wananchi wa kijiji cha Ikoma,wajumbe
wote wa Serikali ya Kijiji,Diwani wa kata ya Ikoma Laulent Adriano.
Mkutano
huo ulikuwa
unazungumzia ajenda ya wanaikoma kunyang’anywa ardhi na mashamba
yao,kulazimishwa kuhama toka kwenye makazi yao pamoja na huhararishwa
kwa wakazi wa Tarime kuchukua mashamba
ya wanaikoma.
Wananchi hao walisema kuwa
licha ya Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa kuwaagiza mbele ya mkutano Wakurugenzi
na Maofisa uhamiaji Wilaya ya Rorya na Tarime kutatua tatizo la mgogoro wa ardhi na kukodishwa kwa
mashamba kwa wageni pamoja na kuhakiki uraia wa wananchi wa Ikoma lakini hadi
sasa hakuna ufatiliaji wala utekelezaji wowote uliofanyika.
Samweli Makori Mjumbe wa
Serikali ya kijiji alisema kushindwakutatuliwa kwa wakati mgogoro wa ardhi wa
wananchi wa Ikoma na kutobainishiwa maeneo halali ya kuishi imepelekea wananchi
wa kitongoji cha Nyamuhunda na Nyanthacho waliovamiwa na nyumba zao kuchomwa moto na mazao
kuharibiwa kubaki kuendelea kuhifadhiwa na wananchi wenzao wa Ikoma jambo
ambalo linalosababisha kushindwa kumudu gharama za kuwahifadhi.
“Baada ya kutokea mapigano baina
ya Waluo na Wakurya tarehe 7-8 tukiwa kwenye mkutano wa wananchi Ikoma mkuu wa
mkoa aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri ya Rorya na Tarime kushughulikia
tatizo la kukodishwa ardhi kwa Wakenya,akawaagiza maofisa uhamiaji kuanza zoezi
mara moja la kuhakiki uraia wa wananchi wa ikoma na wananchi 113 wanaotakiwa
kusajiriwa Ikoma pamoja na wa Nyamuhunda kama njia ya kuwabaini waliomilikishwa
ardhi kinyume cha sheria”alisema Makori.
Aliongeza kuwa”Ajabu mwezi
mzima umekwisha hakuna utekelezaji
wowote mimi mwenyewe nahifadhi watu wawili na familia zao ambao
walifukuzwa kwenye makazi yao na Wakurya wa Tarime na lemewa na mzigo maana
toka mapigano na mali zao kuporwa na kuchomwa moto hawajawahi kupewa msaada
wowote toka Serikalini sasa tunauomba Waziri wa ardhi aje atusaidie huu mgogoro
maana Mkoa nao umeshindwa hata kufatilia
na kuhakikisha wanaikoma wanatatuliwa tatizo la mgogoro wa ardhi
ikishindikana ngazi ya mkoa ninachofata ni Taifa”alisema.
Mwenyekiti wa kitongoji cha
Nyanthcho Gasper Olooch alisema kuwa baada ya RC kumuagiza Mkurugenzi wa
Halimashauri ya Rorya kutatua mgogoro kwa sasa hali si shwari Ikoma kwa madai
kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Rorya Charles Chacha
akiwa ameongozana na Ofisa utumishi na polisi waliwaagiza wananchi wa
kitongoji hicho kubomoa nyumba zao ambapo alitoa siku tatu kufikia tarehe 8
juni mwaka huu wawe tayali wameshabomoa ambapo baaadhi yao walitii agizo na
wengine wamekaidi na waliokubali wanaifadhiwa kwa ndugu zao baaada ya kukosa
mahali pa kuishi.
Pia wananchi walilaani
kitendo cha polisi wa Tarime kwa kitendo cha walichokifanya cha kuwakamata ovyo
wananchi 30 wa kijiji cha Ikoma-Rorya wasiokuwa na hatia akiwemo Diwani wa kata ya Ikoma Laulent Adriano
na Mwenyekiti wa Kijiji na kuwekwa ndani kwa siku 4 katika kituo cha polisi
Sirari-Tarime kwa madai walihusika kufanya uchochezi katika mapigano baina ya
Waluo na Wakurya huku wenzao Wakurya wa kijiji cha Nyamuhunda-Tarime wakisalia
kuwa huru pasipokukamatwa jambo ambalo walisema ni ubaguzi wa kikabila,
No comments:
Post a Comment