MBARONI KWAKUJIFANYA WAGANGA WA KIENYEJI
Na. Luppy
Kung'alo, Polisi Dodoma.
DODOMA JUMATANO JUNE 13- 06 – 2012 : Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa tisa wa utapeli
wanaojifanya Waganga wa Jadi na Tiba Asilia kwa kuwalaghai wananchi katika
vijiji mbalimbali kisha kuwatapeli
na kusababisha hofu, na uvunjifu wa Amani
miongoni mwa wanakijiji mkoani humo.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. Zelothe Stephen
akiwaonyesha waandishi wa habari hawapo pichani vyeti feki vya watuhumiwa wa kundi la Matapeli la LAMBA LAMBA vyeti
hivyo ni vya (UMAWATI )– cha mtuhumiwa DK. Shabani R Kisoma amacho kirefu chake ni UMOJA
WA WAGANGA WATAFITI WA MAGONJWA SUGU UKIMWI
NA TIBA ASILIA TANZANIA, na (CHAUMUTA) –
Cha mtuhumiwa anayejiita DK. Hussein Shomari Mabogo, ambaye amekamatwa , kirefu
chake ni CHAMA CHA UTAFITI WA MAGONJWA SUGU NA UKIMWI KWA TIBA ASILIA.
Pic: Na Luppy Kung’alo
wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen alisema watuhumiwa hao wanajiita
LAMBA LAMBA walikamatwa juzi katika
Wilaya ya Kongwa, katika kijiji cha Mkoka
baada ya Polisi kupata taarifa kuwa, wanakijiji hicho kuwavamia katika
nyumba waliyofikia na kutaka kuwauwa.
Baadhi ya watuhumiwa wa utapeli wa kufanya waganga wa kienyeji wa Kundi la Lamba Lamba wakiwa wameshika dhana za kazi wakiwaonyesha waandishi wa habari pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen hawapo pichani. Kutoka kushoto waliovaa kawaida ni Mkude S/O Mwenda 32 yrs, Mkulima, na Joseph S/O John miaka 27, Mkulima, wote wakazi wa Mkoka – Kongwa na SALEHE S/O OMARI, mwenye umri wa miaka26, mkulima wa Songe Kilindi Mkoani Tanga aliyevaa lubega nyekundu kwa nyeusi na ndani ana fulana mistari.

”Matapeli hawa
wametokea Mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Marogoro, na kuvamia mkoa wetu,
kisha kufanya utapeli wao na kuzusha hali ya hofu na isiyo ya kawaida kwa wanakijiji
wa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma”. Alisisitiza Kamanda Zelothe Stephen.
Aidha Mkuu huyo
wa Polisi Mkoa wa Dodoma alisema, Kundi hilo la LAMBA LAMBA limekuwa likichochea Chuki na Uadui miongoni mwa wanajamii kwa kufanya vitendo
vya kupandikiza vitu nyakati za usiku, halafu baadae mchana wanakwenda kuvifukua na kudai wanabaini
wachawi na kutoa uchawi katika kila nyumba kwa madai ya kualikwa na wazee wa
Kimila.
Kamanda Zelothe
Stephen alisema Matapeli hao, wamedai kualikwa na wazee wa kimila chini ya Mwenyekiti na Katibu waitwao
SAMANDARO S/O? Na CHIPENDWA S/O? Na
kupewa makazi katika nyumba mbili za ukoo wa MAPUGA S/O? Ambazo zinasimamiwa na
Bw. SOSPETER S/O MAPUGA.
Watuhumiwa wa utapeli wa kujifanya Waganga wa Kienyeji na Tiba Asilia wa Kundi la Lamba Lamba wakiwa wameshika dhana za kazi, wakitekeleza amri ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen kuonyesha kile wanachowafanyia wanakijiji mbele ya waandishi wa habari pamoja na Kamanda huyo hawapo pichani.

Akizungumza moja
ya tukio lilozua hofu na kusababisha uvunjifu wa amani alisema katika shuguli
zao walipita kila nyumba katika kijiji walichodai kualikwa na wazee hao lakini walipofika katika nyumba ya MESHACK s/o MAPUGA
aliwakatilia kuingia kwake hivyo waliondoka kwenda katika vijiji vingine.
Alisema Baada ya
kuondoka hapo Mtoto wa Mzee MESHACK S/O
MAPUGA aitwaye MARTHA S/O AINEA MAPUGA MIAKA (34) mgogo mkazi wa kijiji cha
Mlanje alianza kuumwa tumbo kisha kupelekwa zahanati ya Mkoka na hatimaye
Hospitali ya wilaya Kongwa ambapo madaktari walithibitisha kifo cha binti huyo
kutohusiana na imani za kishirikina lakini kwa bahati mbaya alifarikia dunia
usiku wa tarehe 10/06/2012 akiwa Hospitalini hapa.
Watuhumiwa wa utapeli wa kujifanya Waganga wa Kienyeji na Tiba Asilia wa Kundi la Lamba Lamba wakiwa wameshika dhana za kazi, wakitekeleza amri ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen kuonyesha kile wanachowafanyia wanakijiji mbele ya waandishi wa habari pamoja na Kamanda huyo hawapo pichani.
Watuhumiwa wa utapeli wa kujifanya Waganga wa Kienyeji na Tiba Asilia wa Kundi la Lamba Lamba wakiwa wameshika dhana za kazi, wakitekeleza amri ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen kuonyesha kile wanachowafanyia wanakijiji mbele ya waandishi wa habari pamoja na Kamanda huyo hawapo pichani.
”Kifo hicho
kilileta sintofahamu katika familia hiyo, iliyopelekea kufikiri kwamba kikundi
cha LAMBA LAMBA walihusika na kwamba
ndio tatizo kwa sababu za imani kishirikina.”aliongeza Bw, Zelothe
Stephen.
Mkuu huyo wa
Polisi wa Mkoa wa Dodoma alisema kutokana na hali hiyo wanakijiji waliungana na familia ya wafiwa na
kwenda kuwavamia kundi la LAMBA LAMBA wakiwa na silaha za jadi, ambazo ni mikuki,
mapanga na marungu kwa lengo la kutaka kuwaua lakini walifanikiwa kuvunja
mlango na madirisha na kukuta wametoroka.
Baadhi ya
wanakijiji walitoa taarifa za tukio hilo kwa Jeshi la Polisi na Operesheni ya kuwatafuta watu hao ilianza ambapo jumla ya watuhumiwa saba kati ya tisa
wa kundi hilo walikamatwa usiku huo na
wengine wawili walikamatwa siku iliyofuta wakiwa wanawafuatilia wenzao, alisema
Kamanda Zelothe.
Bw. Zelothe Stepen alisistiza kwamba pindi upelelezi utakapo kamilika watuhumiwa hao watafikishwa
mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Hata hivyo
Kamanda Zelothe alisema, Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeunda Kikosi kazi
Maalumu katika wilaya zake zote kwa lengo la
kufanya Operesheni Maalum ili
kudhibiti na kutokomeza kundi hilo na
washirika wake na kuahidi kuwasiliana na
Makamanda wenzake wa mikoa ili kudhibiti vitendo hivyo.
”Napenda kutoa
wito kwa wananchi wote, viongozi wa Serikali katika ngazi za Vijiji, Kata,
Tarafa na Wilaya kusimamia Sheria,
Kanuni na taratibu za nchi zinavyotaka, ili kuweza kudhibiti uhalifu huu
na kuondoa hali ya sintofahami miongoni
mwa jamii inayoweza kusababisha uvunjifu
wa Amani ndani na nje ya mkoa wa Dodoma inatokomezwa.” Alisistiza kamanda
Zelothe Steven
No comments:
Post a Comment