AJARIBU KUJINYONGA KWA WEMBE
Na Dinna Maningo,Tarime
MKAZI wa mjini Tarime Mkoani Mara Francis Marwa (65) amenusurika kifo katika jaribio la kutaka kujiua kwa kujikata shingoni na wembe.
Na Dinna Maningo,Tarime
MKAZI wa mjini Tarime Mkoani Mara Francis Marwa (65) amenusurika kifo katika jaribio la kutaka kujiua kwa kujikata shingoni na wembe.
Tukio hilo lilitokea juni,10,2012 majira ya saa mbili Asubuhi Nyumbani kwake huko mji mdogo wa Sirari.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya Tarime Malco Nega alisema walipokea majeruhi huyo juni 10,2012 majira ya mchana akiwa na jeraha shingoni ambalo limekatwa na wembe.
Nega alisema kuwa mgonjwa huyo amelazwa wod ya wanaume no (3) Hospitalini hapo akiendelea kupatiwa matibabu.
Nega alifafanua kuwa hali ya mgojwa huyo inaendelea vizuri na punde itakapopata nafuu ataruhusiwa kurudi nyumbani kwake.
Mzee Marwa alipohojiwa na gazeti hili kuhusu sababu ya yeye kujaribu kujidhuru na kutaka kuondoa uhai wake kwa kutumia wembe alisema kuwa amegadhabika na familia yake kutompeleka kwa shemeji yake Dar es salamu ili shemeji yake ampeleke kwa mganga wa kienyeji Sumbawanga kwa matibabu ya moyo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa mda mrefu.
Marwa aliongeza kuwa hata kama watampa ulinzi kiasi gani punde atakapopata mwanya wa kupata kamba ni lazima atajinyonga tu.
No comments:
Post a Comment