Na. Luppy Kung’alo, Dodoma
DODOMA JUMANNE JUNI
12, 2012. Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawasaka Watu
wawili kwa tuhuma za Unyang’anyi wa
kutumia nguvu baada ya kuwatisha kwa
jambia wasichana wawili raia wa Uholanzi na kisha
kuwapora vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni moja laki
mbili na sitini na nne elfu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Bw. ZELOTHE STEPHEN alisema Tukio hilo lilitokea muda wa saa saba na
dakika arobaini na tano mchana katika eneo
la area D Wilaya ya Dodoma Mjini, Karibu
na nyumba inayojengwa kwa ajili ya 0fisi na Makazi ya Mh. Waziri Mkuu
Bw. MIZENGO KAYANDA PETER PINDA.
Alitaja vitu vilivyoporwa
katiika tukio hilo kuwa ni Kamera ya digitali aina ya Canon, Simu mbili za
mkononi aina ya Nokia na Samsung, Begi la Mgongoni, Viatu vya wazi pea mbili
(Sandal) Taulo la Hostel, Sketi, Wallet na Pesa za kitanzania shilingi 40,000/=.
Aidha aliwataja Waathirika wa Unyang’anyi huo kuwa ni wa LISA D/O LEMEN
mwenye umri wa miaka (19) na FLEUR D/O EDITH SCHOLTEN Mwenye Umri wa miaka (17)
wote ni Raia wa Uholanzi ambao wako nchini kama waalimu wa shule ya msingi na sekondari ya Saint Germa
iliyoko jijini Arusha inayofundisha watoto ambao wazazi wao wamefungwa gerezani.
“Raia hao wa Uholanzi ambao
walikuja kutembea Mjini Dodoma wakitokea Arusha walifikia katika Hostel ya
Saint Maria ambayo wanaishi wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule za
kutwa za mjini Dodoma”:
Kamanda ZELOTHE STEPHEN
alisema kuwa wageni hao walioporwa vitu hivyo, baada ya kufika katika eneo hilo wakiwa
na mwenyeji wao aliyejulikana kwa jina la Sister PONSIAN PROTAS MATAKA miaka
(43) ambaye anaishi katika Hostel waliyofikia wageni hao ya Saint Maria ilyopo
eneo la Uhindini.
Alisema walipofika katika eneo hilo ambalo lina mlima kwa lengo la kupiga
picha walimkuta mlinzi wa eneo hilo na Sister PONSIAN akamuuliza mlinzi kuhusu usalama wa eneo hilo
akajibiwa shwari ndipo akawaacha wageni wake hao waendelee na shuguli
iliyowapeleka hapo.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Jeshi la Polisi, Bw. ZELOTHE STEPHEN alisema wakiwa katika shughuli zao, walitokea vijana
wawili wasio wafahamu wakiwa na Jambia
na kuwataka kutoa kila kitu walichokuwa nacho, na ndipo mmoja wa
watuhumiwa akawasachi na kupora vitu
hivyo kisha kutokomea kusikojulikana.
Kamanda huyo wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Dododma alisema kwamba jeshi lake limeanzisha msako mkali kuhusiana na tukio
hilo na pia kutoa wito kwa waananchi
wanaoishi karibu na eneo husika pamoja
na wananchi wote kwa ujumla, kwa kupitia
mkakati wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kushirikiana kwa kutoa taarifa za uhalifu na
wahalifu ili kwa pamoja kuweza kuzuia vitendo vya uhalifu katika maeneo yao.
Wakati huo huo jeshi la
Polisi mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa
thelathini na nane kwa makosa
mbalimbali ya uhalifu ikiwemo Pombe ya Moshi Lita (38), Mitambo mi nne ya
kutengenezea gongo, Vipodozi mbalimbali Vilivyopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu pamojana misokoto Mitano ya
Bhangi katika yilaya ya Dodoma Mjini.
MWISHO:
No comments:
Post a Comment