Dinna Maningo,Tarime
WANANCHI WA Kijiji cha Kerende Kata ya
Kemambo-Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara wameamua kuanzisha ulinzi
shirikishi kama njia ya kupunguza matukio yanayojitokeza ya mara kwa mara
ya uvamizi wa kutumia silaha pamoja
na uporaji wa mali za wananchi ndani ya kijiji hicho.
Ulinzi huo umehalalishwa na
wananchi kufanyika rasmi leo ambapo kila kitongoji kitapaanga ratiba kwa majina
na siku ya watu kwenda kwenye malindo pamoja na kudhibiti njia ambazo ni
hatarishi ambapo zoezi hilo la ulinzi limepangwa kuanza usiku wa saa moja hadi
saa 12 asubuhi,ambapo waliadhimia kuwa kwa wale ambao hawatofika kuimalisha
ulinzi watatozwa faini ya sh.50,000 kwa kila mmoja kwa siku moja.
Hayo yalibainika kwenye Mkutano
wa wananchi uliohitishwa na mwenyekiti wa Kijiji cha Kerende Mambaga
Mhamed kwa ajili ya kuzungumzia hali ya
ulinzi na usalama wa kijiji na namna ya kudhibiti matukio ya uhalifu kijijini
hapo.
Mkutano huo uliofanyika
viwanja vya shule ya msingi Kerende ulihudhuliwa na wananchi wa kijiji cha
Kerende, wenyeviti wa vitongoji,Diwani wa Kata ya Kemambo Wilson Mangure,viongozi
mbalimbali wa jeshi la polisi akiwamo Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi
Nyamwaga Simion Maigwa na mkuu wa kituo cha Polisi Nyamongo Kibori Ntinginya.
Wananchi hao walisema kuwa
kijiji cha Kerende kimekuwa na wimbi la majambazi wanaovamia nyumba za watu na
kupora mali na kisha kujeruhi watu mbalimbali hali ambayo imesababisha wananchi
kuishi bila amani kwa kuhofia usalama wa maisha yao na mali zao.
“Kijiji cha Kerende hakuna
amani watu tunaishi kwa hofu watu wanavamiwa njiana kwenye majumba yao
wanaporwa pesa na mali majambazi wanavamia kwa risasi na kujeruhi watu tumekuwa
kama mizoga ili jeshi lifanikiwe vizuri lazima lijipange liwe na silaha za
kutosha za kukabiliana na adui kwahiyo wananchi tunaomba kila mwanaume anunue
mkuki na upinde tuanzishe ulinzi wateuliwa watu kwa ajili ya kuzunguka kwenye
maeneo ili jambazi anapokuja tunamkabili mara moja vinginevyo tutakufa maana
wanasimamisha magari wananshusha watu na kuwapora na kuwajeruhi wengine
wanafatwa majumbani wanapigwa”alisema Mwananchi Nyamuhanga Kiguku
Stiven Ndeti alisema kuwa kuendelea
kuwepo kwa vitendo vya ujambazi na uporaji ni baada ya kupokelewa watu na
kuruhusiwa kuishi kijijini ambao walifukuzwa na kijiji kwa kutokuwa na imani nao,
ambapo walitaka watu hao waliofukuzwa na kijiji na kisha kurejea wakamatwe na
kupeleka mahakamani kwa madai kuwa ndio wanaendelea kufanya matukio
yanayohatalisha usalama wa wananchi.
Mtendaji wa kijiji cha
Kerende Marwa Nyamuhanga aliongeza kuwa kusema kuwa sababu nyingine ya kuwepo
kwa vitendo viovu inatokana na ongezeko la maitruda wanaoingia mgodini kwa nia
ya kuokota mawe ya dhahabu ambapo alisema kuwa baadhi yao ujihusisha na vitendo vya ujambazi na
uporaji kwenye nyumba za watu nyakati za usiku
Juma Mturu aliwalalamikia
wenyeviti wa vitongoji kwa kutotekeleza majukumu yao ya kuimalisha ulinzi na
usalama na kwamba wamekuwa si
wafatiliaji katika kuwabaini wageni ambao ukaribishwa na wananchi nao kwa siri
bila kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji
ambapo alimtaka kila mwananchi anapofikiwa na mgeni kutoa taarifa kwa
mwenyekiti ili watambue mahali alikotoka
na nia yake ya kufika kijijini.
Kibwaba Nyamuhanga alisema kuwa kuendelea kuwepo kwa vitendo vya
ujambazi vinatokana na wananchi kutokuwa na ushirikiano katika kuwataja wale
wote wanaojihusisha na vitendo viovu ili wachukuliwe hatua za kisheria badala
yake wamekuwa wakificha maovu hali inayosababisha kutokuwepo kwa amani ya kutosha.
“amani inapokosekana
tunashindwa kufanya shughuli za maendeleo tuhimizane ulinzi kwenye vitongoji
iwepo ratiba ya ulinzi uhalifu umezidi
ulinzi wetu ni sisi wenyewe tusitegemee kuwa kuna mtu atalinda mali zetu inabidi tujipange tukubaliane tuchukuwe
dharura ya kuanzisha ulinzi shirikishi nashangaa kuna watu wana bunduki zisizopungua
tano lakini hizo bunduki hazitusaidii majambazi wanakuja na wanaiba lakini wao
wamekaa nazo ndani hazina msaada wowote kwa wananchi”alisema Nyamuhanga.
Mkuu wa polisi Wilaya ya
Kipolisi Simion Maigwa aliunga mkono hatua hiyo ya wananchi kuanzisha ulinzi
shirikishi ambapo alisema jambo hilo ni jema
kwani litasaidia kupunguza matukio ya uhalifu ambapo alikitaka kila kitongoji kutunga
sheria ndogondogo za kijiji ili kufanikisha zoezi hilo la ulinzi shirikishi
“Nijambo jema kuanzisha
ulinzi shirikishi ulinzi uanzishwe kwa kila kitongoji ikiwa ni pamoja na
kudhibiti mapito ya njia tungeni sheria ndogondogo za kijiji kwa wale ambao
hawataenda kwenye lindo,lakini pia mjenge mahusiano mazuri baina ya kijiji cha
Genkuru na Kerende hamna mahusiano
mazuri hali inayosababisha kufanyiana uharifu kuibiana mifugo kwa sababu tu ya
kutokuwepo kwa mahusiano mema yanayosababisha kujengeana fitina na kulipizana
visasi”alisema Maigwa
Mkuu wa kituo cha polisi
Nyamongo Kibori Ntinginya alisema kuwa kumekuwa na tatizo la usafiri wa gari la
polisi ambao umekuwa ukisababisha polisi kutofika kwa muda unaotakiwa eneo la
tukio ambapo alisema kuwa kituo chake cha Nyamongo kina gari moja la polisi ambalo
hutakiwa kutoa huduma zote ndani ya vitongoji na vijiji vyote vilivyo ndani ya
mji wa Nyamongo na hivyo gari hilo kujikuta kutowafikia wahitaji wote hali
ambayo inasababisha kuwepo kwa malalamiko baina ya wananchi na msaada wa jeshi
la polisi ambapo pia gari hilo utumika pia kuwapeleka watuhumiwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment