Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa ajili ya Sierra Leone leo
imetoa adhabu ya kifungo cha miaka 50 jela kwa dikteta wa zamani
wa Liberia, Charles Talyor.
Akisoma hukumu hiyo muda mchache
uliopita, Jaji Richard Lussick amesema kwamba jopo la majaji
limeamua kwamba Taylor atatumia kifungo chake kwa awamu moja.
Mahakama hiyo ilimtia hatiani Taylor mwenye umri wa miaka 64,
hapo mwezi Aprili.
Taylor alipatikana na makosa ya kuwafadhili na
kuwapa silaha waasi wa United Revolution Front (URF) wa nchi jirani
ya Sierra Leone wakati nchi hiyo ikiwa kwenye vita vya wenyewe
kwa wenyewe. Katika vita hivyo vya baina ya mwaka 1992 na 2002,
kiasi ya watu 120,000 waliuawa.
Wakili wa upande wa mashtaka
amemba kifungo cha miaka 80 dhidi ya Taylor. Kesi yake iliyoanza
mwaka 2007 ilishuhudia watu kadhaa maarufu wakihusika, akiwamo
mwanamitindo wa Kimarekani, Naomi Campbell, ambaye alisimama
kizimbani kama shahidi.
Kesi hiyo ilihamishiwa kutoka Afrika ya
Magharibi na kufanyika nchini Uholanzi kwa sababu za kiusalama.
No comments:
Post a Comment