SERIKALI ITAENDELEA KUYAUNGA MKONO MASHIRIKA YA MISAADA KWA WANANWAKE
Na. Mohammed Mhina, Zanzibar
Serikali
imesema itaendelea kuunga mkongo juhudi zozote zitakazosaidia kumkomboa
mwanamke kielimu ili kujenga moyo wa kujiamini katika nafasi ya
uongozi.
Ahadi hiyo imetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma Mh.
Cellina Kombani, wakati akifungua mafunzo ya wiki moja kwa wanawake wa
mikoa ya Zanzibar na Dar es Salaam yanayofanyika mjini Zanzibar.
Wakati
akifungua mafunzo hayo yanayotolewa na Shirika la Misaada la Ujerumani
la Hanns Sedel Foundation Mh. Kombani amesisitiza kuwa hatua
inayochukuliwa wa shirika hilo hapa nchini, amesema serikali inaunga
mkono hatua hiyo ambayo amesema itamuwezesha mwanamke kujenga moyo wa
kujiamini.
Waziri Kombani akiongea na washiriki hawapo pichani
Ameviomba vyama vya siasa hapa nchini
kuwasaidia wanawake katika kuwapa wanawake fursa ya kushiriki katika
mafunzo kama hayo ili kuwajengea wanawake uwezo wa kujiamini na
kutekeleza majukumu yao ya uongoozi katika ngazi mbalimbali.
Shirika
la Misaala la Hanns Seidel Foundation lenye makao yake makuu katika
Jiji la Munich nchini Ujerumani, kwa ushirikiano na Kituo cha utawala
bora na maendeleo ya kiuchumi wameandaa mafunzo kwa wanawake hapa nchi.
Waziri Kombani akiongea na washiriki hawapo pichani
Zaidi ya wanawake 160 watanufaika na mafunzo yatakayoendeshwa katika kanda sita zitakazoishirikisha mikoa yote hapa nchini.
ataobias Mapesi mkurugenzi wa Kituo cha utawala bora na maendeleo ya kiuchumi
Hayo
yamebainishwa na Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Hanns
Seidel Foundation nchini Tanzania Bw. Konrad Teichert wakati wa ufunguzi
wa mafunzo kwa akina mama katika kituo cha Zanzibar ambapo mgeni rasmi
alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma Mh. Cellina Kombani.
Kaimu
Mkurugenzi wa kituo cha utawala bora na maendeleo ya kiuchumi hapa
nchini Bw. Tobias Mapesi, amezitaja kanda hizo kuwa ni Dar es Salaa
yenye mikoa ya Dar es salaam yenyewe, Pwani na Lindi.
No comments:
Post a Comment