MGOMO WA WAAUGUZI MUSOMA WASHINDWA KUPATA SULUHU
Baadhi ya wauguzi wakiwa wametulia katika eneo la maengesho ya magari kufuatia mgomo wa wauguzi Hospital ya mkoa wa Mara
Mgonjwa ambaye alifikishwa hospitalini hapo akiwa amepigwa panga na mpenzi wake lakini mpaka tunaondoka eneo hilo hakuna huduma ambayo alikuwa amepata
Katibu Tawala wilaya ya Musoma Bi Dora Makinga alifika akiwa anamwakilisha mkuu wa mkoa wa Mara lakini hakufanikiwa kuwatuliza kwani wao walitaka fedha na c maneno
Katibu wa TUGHE mkoa wa Mara bw Lushakuzi akiwa mstari wa mbele kuwatuliza wauguzi hao
FROM BINDA NEWZ
Wauguzi
katika hospitali ya Mkoa wa Mara wameweka mgomo wa kuingia wodini na
kutoa huduma mbalimbali katika hospitali hiyo wakishinikiza uongozi wa
hospitali hiyo kuwalipa madai yao mbalimbali ambayo wanadai na kusema
kuwa hawatafanya kazi mpaka hapo watakapo tekelezewa.
Mgomo huo
wa wauguzi umeanza leo asubuhi baada ya wauguzi hao kufika kazini na
kushindwa kufanya kazi huku wakisema kuwa wamenyanyaswa vya kutosha na
wanachotaka nikulipwa madai yao ndipo huduma kutoka kwao ziweze
kuendelea katika hospitali hiyo.
Kutokana na mgomo huo
kumesababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa wa wodini na wale wa nje
baada ya kukosa huduma mbalimbali huku wengine wakitupia lawama kwa
uongozi wa hospitali hiyo kwa kushindwa kukaa na wauguzi hao na kufika
muafaka ili waendelelee kupata huduma kama kawaida.
Mmoja wa
wauguzi wa hospitali hiyo Antunia Machibula alisema kuwa kutokana na
kushindwa kuthaminiwa kutokana na kupuuzwa kwa malipo yao na shughuli
wanazozifanya wameamua kufanya hivyo ili kushinikiza kulipwa malipo yao
wanayoyadai na kusema kuwa malipo wanayodai tayari yalishatolewa kutoka
katika ofisi za ngazi ya juu zinazohusika.
Amesema kuwa baada
ya kutokea mgomo wa madaktari miezi michache iliyopita ofisi ya Waziri
Mkuu ilifanya malipo yote yanayohusiana na madaktari na waauguzi lakini
cha kushangaza wao wameshindwa kulipwa huku wengine wakilipwa kiwango
ambacho akistahili katika malipo yaliyokuwa yamekokotolewa.
"Kwa mfano yule muuguzi ambaye anatakiwa kulipwa malipo ya ziada ya
shilingi elfu kumi analipwa shilingi elfu tano na yule anaetakiwa
kulipwa shilingi shilingi elfu ishilini analipwa elfu kumi sasa hii
sisis tunaona ni manyanyaso kwetu na tunaomba jamii ituelewe hivyo maana
tumechoka kunyanyaswa",alisema Machibula.
Kwa upande wake
muuguzi Juma Warioba alisema kuwa ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa kiasi cha
shilingi milioni 40 kutokana na madai mbalimbali yanayowahusu lakini
wanashangazwa na kutokulipwa kama inavyostahili licha ya kukaa vikao
mbalimbali kuzungumzia suala hilo na kilichobaki ni kutokufanya kazi
mpaka pale madai yao yatakaposikilizwa.
Baada ya maelezo hayo
ya wauguzi wa hospitali hiyo ya Mkoa wa Mara kueleza madai yao BINDA
NEWS lilifika katika ma wodi ya hospitali hiyo na kukuta wagonjwa wakiwa
pekee yao huku kukiwa hakuna huduma mbalimbali zinazoendela za
kimatibabu na kulalamikia kile ambacho kilikuwa kikiendelea katika
hospitali hiyo.
Mmoja wa wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika
wodi namba saba aliyejitambulisha kwa jina la Musa Mikidadi alisema
tangu asubuhi ajapata huduma yeyote licha ya kutakiwa kupata huduma
kutwa mara tatu na kudai kuwa kuna mmoja wa wagonjwa jamaa zake
walilazimika kumtoa nje ya wodini na kwenda kutibiwa katika vituo
binafsi.
Sakata lingine likatokea katika chumba cha kuhifadhi
maiti katika hospitali hiyo baada ya muhudumu wa chumba hicho nae kuweka
mgomo wa kutoa wala kupokea maiti katika chumba hicho kwa kuwa kufanya
hivyo ni sawa na kuwasaliti wenzake kwa kuwa wote wapo katika mgomo wa
madai ya kimaslahi.
Muhudumu huyo aliyejitambulisha kwa jina
la Masatu Masatu alisema kuwa hataweza kufanya kazi yeyote mpaka hapo
utakapapatikana muafaka ambao wanaudai kutoka kwa viongozi licha ya
kuwepo kwa watu waliokuwa wakihitaji huduma ya kuwatoa ndugu zao katika
chumba hicho cha kuhifadhia maiti.
Kutokana na sakata hilo
kulipikea katibu tawala wa wilaya ya Musoma ambaye ni kaimu mkuu wa
Wilaya ya Musoma kufika katika hospitali hiyo akiwa na kamati ya ulinzi
na usalama ya Wilaya Debora Makinga ili kuzungumza na wauguzi hao
lakini hadi majira ya saa 8;40 alasiri kulikuwa hakujapatikana muafaka
wowote kati ya wauguzi na viongozi hao.
No comments:
Post a Comment