MAJAMBAZI YAUA ASKARI POLISI KIGOMA
Na Pardon Mbwate na Felister Chubwa wa Jeshi la Polisi Kigoma
Askari
Polisi mmoja mkoani Kigoma mwenye namba D.1645 Stafu Sajenti S/SGT
George Luzegama(53), ameuwa kwa kupigwa risasi na majambazi.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Francis Mwakabana, amesema kuwa
tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 3.30 usiku huko kwenye eneo la
Mwanga Kitambwe mjini Kigoma ambapo majambazi yakiwa na sihala aina ya
short Gun walimpiga risasi askari huyo mwenye namba D.1645 S/SGT George
Luzegama(53).
Kamanda
Mwaakabana amesema askari huyo alipigwa risasi kwenye mbavu za upande
wa kushoto alipokuwa kwenye duka moja la madawa ambapo majambazi
walikuwa wamevamia hapo na walimshambulia wakidhani ni miongoni mwa
askari walioweka mtego wa kuwanasa.
Askari
huyo alifariki muda mfupi mara baada ya kufikishwa wakiwa katika
Hospitali ya Maweni mkoani Kigoma alipokuwa akipatiwa matibabu.
Katika
tukio hilo, majambazi hayo yalipora kiasi cha fedha za mauzo kutoka
kwenye duka hilo na baadaye walikimbia kutokomea pasikojulikana na
Polisi inaendelea na msako dhidi ya majambazi hayo.
Katika tukio hilo, muuzaji wa duka hilo Bi. Rehema Gwimo(30), alinusurika na anaendelea kuisaidia Polisi katika upelelezi wa tukio hilo.
Huyo
ni askari wa nne kufariki mkoani Kigoma katika kipindi kisichozidi
miezi miwili ambapo askari wawili walifariki dunia kwa ajali ya pikipiki
na mwingine kuuawa na majambazi wakati wa mapambano kwenye ziwa
Tanganyika.
KATIKA TUKIO LINGINE Katika
tukio linguine, Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linamsaka mwananfunzi
mmoja wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Mwike mjini Kigoma
Bi. Rehema Issa(22) ambaye ni mkazi wa eneo la Kamara kwa tuhuma za
kujifungua na kukitumbukiza kichanga chake chooni.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo SSP Francis Mwakabana,
amesema kuwa kichanga hicho ambacho kiliokolewa na wanafunzi wa shule
mmoja ya msingi kikiwa hai lakini kilifariki muda mfupi wakati
kilipokuwa kikipelekwa Hospitalini kwa matibabu.
No comments:
Post a Comment