SERENGETI
Mwanaume mmoja wa wilaya ya Tarime mkoani Mara,anadaiwa kuitelekeza
familia yake yenye watoto wanne walemavu aliowazaa na mke wake wa ndoa
kwa madai
ya kukwepa mkosi, jambo ambalo limemlazimu mwanamke huyo
kuishi maisha ya kutegemea misaada ya majirani kwa ajili ya mahitaji ya
watoto wake.
Bi Esther Chacha mkazi wa kitongoji cha
Songambele kata ya Sabasaba wilayani Tarime,amesema baada ya kuzaa
watoto watano, wanne wakiwa ni walemavu, mme wake huyo ambaye amemtaja
kwa jina la Chacha Merengo,aliikimbia familia hiyo na kuoa mke mwingine
kisha kwenda kuishi mjini Mugumu Wilayani Serengeti,kwa madai kuwa
hawezi kutunza watoto wasio na faida.
Aidha mama huyo ameiomba
Serikali na wasamalia wema, kumsadia kutunza watoto hao wenye ulemavu
ikiwa ni pamoja na kumsomesha mtoto mmoja ambaye amebahatika kuzaliwa
bila ya kuwa na ulemavu katika familia hiyo,ambaye kwa sasa anasoma
darasa la saba katika shule ya msingi ya Mturu katika kata ya Rebu
ambayo imekuwa akihitunza tangu mwaka 2005 alipachwa na mme wake
Nao baadhi ya majirani wa mama huyo,Bi Esther Eliah na Bi Rose
Yohana,wameomba watu ambao wataguswa na mateso anayopata mama huyo
katika kulea watoto hao kutoa msaada ambao utamuwezesha kuwatunza
watoto wake.
Hata hivyo mme wa mama huyo Bw Chacha
Merengo,alipotafutwa kwa njia ya simu kwa zaidi ya
mara nane ili kuthibitisha madai hayo hakuweza kupatikana kutoka na simu
yake ya mkononi muda wote kuwa imezimwa na juhudi za kumtafuta bado
zinaendelea.
No comments:
Post a Comment