Friday, January 13, 2012

YALIYOJIRI MUSOMA LEO NA MIKOA JIRANI


MUSOMA


WANANCHI MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA WAMETAKIWA KULIPIA VIWANJA VYAO ILI KUEPUKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA KUVITWAA VIWANJA HIVYO.

AKIONGEA KATIKA KIPINDI CHA BIG BREAKFAST LEO ASUBUHI  AFISA ARDHI MANISPAA YA MUSOMA JACKSON MAGESA AMESEMA KUWA HALAMSHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA IPO NYUMA KATIKA MAKUSANYO YANAYOTOKANA NA KODI YA VIWANJA KULIKO HALMSHAURI YA WILAYA YA TARIME.

AMESEMA PAMOJA NA MANISPAA YA MUSOMA KUONEKANA IMEJITANUA KATIKA SEHEMU KUBWA LAKINI MAKUSANYO YA VIWANJA YANAKUWA HAFIFU IKILINGANISHWA NA TARIME AMBAYO HAJAJITANUA.

AFISA ARDHI HUYO AMESEMA KUWA KWASASA WANANCHI WA MANISPAA YA MUSOMA WANATAKIWA KUCHANGIA KIASI CHA SHILINGI LAKI MBILI KATIKA KUPIMA VIWANJA MAENEO YA NYAMIHONGO, BWERI, BUHARE NA SONGAMBELE AMBAPO PIA BAADAYE WATALIPA FIDIA.

KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI MARA KWA MARA KATIKA MANISPAA YA MUSOMA AFISA ARDHI HUYO AMESEMA KUWA TATIZO HILO LINATOKANA NA WANANCHI WENGI KUTOJUA SHERIA YA ARDHI.

AMEONGEZA KUWA UFINYU WA BAJETI NDIYO KIKWAZO CHA OFISI YAKE KUSHINDWA KUTOA ELIMU INAYOHUSIANA NA SHERIA YA ARDHI KATIKA MANISPAAM YA MUSOMA, AIDHA AKIJIBU MASWALI ALIYOWEZA KUULIZWA KUPITIA VICTORIA FM AFISA AMESEMA TATIZO NI WANANCHI KUTOJUA SHERIA

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,


SERIKALI MKOANI MARA,IMESEMA KUWA PAMOJA NA IDADI KUBWA YA WATAZANIA KUTEGEMEA KILIMO KATIKA KUJIKOMBO KIUCHUMI  NA KUCHANGIA UCHUMI WA NCHI LAKINI KUTOKUWA NA UWEZO WA KUMUDU UNUNUZI WA ZANA ZA KISASA ZA KILIMO KUMECHANGIA KUDHOTESHA SEKTA HIYO.
KUTOKANA NA HALI HIYO IMEWAFANYA WANANCHI KULIMA KILIMO CHA KUJIMU TU KWAAJILI YA KUKABILIANA NA NJAA BADALA YA KILIMO CHA BIASHARA,HIVYO KUWAFANYA KUENDELEA KUWA NA MAISHA DUNI KIMAISHA.
KAULI HIYO IMETOLEWA NA KAIMU MKUU WA MKOA WA MARA KAPTENI MSTAAFU GEOFREY NGATUNI WAKATI AKIZUNGUMZA NA WABUNGE 18 KUTOKA KATIKA SERIKALI YA SWIDEN AMBAO WAKO NCHINI KWA LENGO LA KUANGALI HALI YA MAENDELEO YA WAKULIMA NA NI JINSI GANI WATANZANIA WANAVYOJIKITA KATIKA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI
AMESEMA KUWA HALI HIYO KWA WAKULIMA INATOKANA NA WAKULIMA WALIO WENGI KUWA NA HALI DUNI YA MAISHA NA KWAMBA HATA WALE WAKULIMA WALIO NA UWEZO WA KULIMA KILIMO CHA BIASHARA WAMEKUWA WAKITHIRIWA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI HIVYO KUKATA TAMAA YA KUENDELEZA KILIMO.
AIDHA AMESEMA KUWA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI IMEJIWEKEA MALENGO YA KUHAKIKISHA INAPANDA MITI ISIYOPUNGUA MILIONI  1.5 KWA NCHI NZIMA.
AMESEMA AMESEMA KUWA ZOEZI HILO LA UPANDAJI WA MITI LIMEKUWA LIKISIMAMIWA NA SERIKALI LAKINI MITI HIYO INAKUWA NI MALI YA WANANCHI WENYEWE HUKU AKISISITIZA MIPANGO YA SERIKALI YA KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA KATIKA KUHAKIKISHA WANALIMA KILIMO CHA MANUFAA NA KISICHOKUWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA.
KWA UPANDE WAKE MKUU WA KITENGO CHA WATAALAMU WA MAENDELEO YA TAASISI  VI  AGROFOREST  BI LUCY RWEGASIRA,AMESEMA KUWA MWAKA HUU NI MWAKA WA USHIRIKA DUNIANI HIVYO UJIO WA WABUNGE HAO PIA UMELENGA KUANGALIA NI JINSI GANI TANZANIA IMEJIANDAA KATIKA KUADHIMISHA MAADHIMISHO HAYO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,


MWANZA


MBUNGE WA JIMBO LA NYAMAGANA JIJINI MWANZA EZEKIEL WENJE AMESEMA KUWA AMEPOKEA KWA FURAHA NAFASI ALIYOTEULIWA NA CHAMA CHAKE CHA UKURUGENZI WA MAHUSIANO WA KIMATAIFA.

AKIONGEA NA VICTORIA FM KWA NJIA YA SIMU LEO JIONI MH WENJE AMESEMA KUTEULIWA KATIKA NAFASI HIYO NI HESHIMA KWA JIMBO LA NYAMAGANA, VIJANA WALIOPO KATIKA CHAMA HICHO NA PIA KWA FAMILIA YAKE.

AMESEMA ANAAMINI UWEZO ANAO KATIKA KUTEKELEZA KAZI HIYO HIVYO ANAAMINI ATASHIRIKIANA VYEMA NA WANACHAMA WA CHAMA CHA CHADEMA.

KUHUSU CHANGAMOTO NDANI YA JIMBO HILO MH WENJE AMESEMA KUWA AMEJITAHIDI KUPUNGUZA CHANGAMOTO ZILIZOKUWA ZIKILIKABILI JIMBO HILO HASA KATIKA SUALA LA ELIMU, AMESEMA AMEFANIKIWA KUGAWA MADAWATI 500 KATIKA JIMBO HILO.

MH WENJE AMESEMA KUWA ANAAMINI ATAKUWA MBUNGE TANZANIA KUMALIZA TATIZO LA MADAWATI KATIKA JIMBO LAKE HUKU AKIWAASA WANASIASA KUACHA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI KUTATUA MATATIZO YAO

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

DAR ES SALAAM


CHAMA CHA NCCR MAGEUZI KIMESEMA KUWA HAKITAUNGA MKONO MAMALAKA YA NISHATI NA MAJI NCHINI EWURU JUU YA KUPANDISHA GHARAMA ZA UMEME,

AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM MKUU WA IDARA YA KAMPENI YA CHAMA HICHO FAUSTINE SUNGURA AMESEMA KUWA KUFANYA HIVYO KUTASABABISHA KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA KWA MWANANCHI.

SUNGURA AMESEMA KUWA MBALI NA KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA KWA MWANANCHI PIA GHARAMA ZA UZALISHAJI ZITAKUWA JUU IKILINGANISHWA NA KIPINDI KILICHOPITA.

MKURUGENZI HUYO AMEONGEZA KUWA UHALIBIFU WA MAZINGIRA UTAONGEZEKA KATIKA JAMII KWANI WATU WATASHINDWA KUTUMIA GESI NA HIVYO KUTUMIA MKAA KATIKA MATUMIZI YAO.

AMESEMA KATIKA SOKO LA USHINDANI BIDHAA ZA TANZANIA ZITASHINDWA KUNUNULIWA KATIKA SOKO LA AFRIKA MASHARIKI KUTOKANA NA BIDHAA HIZO KUWA GHARAMA YA JUU IKILINGANISHWA NA NCHI YA KENYA AMBAYO ILISHUSHA GHARAMA ZA UMEME KWA ASILIMIA 5 HUKU TANZANIA IKIPANDISHA KWA ASILIMI 40

AIDHA MKURUGENZI HUYO WA KAMPENI WA NCCR MAGEUZI  AMESEMA KUWA CHAMA CHAKE KIMEKUSUDIA KUKATAA RUFAA TUME YA USHINDANI IFIKAPO JANUARY 20,2012

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment