Saturday, January 14, 2012

HABARI NA MWANA WA AFRIKA FRM MUSOMA

BUNDA

KITUO cha kuwajengea wananchi uwezo kuhusu haki za binadamu cha CARH cha mjini Bunda mkoani Mara,kimelaani kitendo cha wananchi wa kijiji cha Mwibagi katika halmashauri ya Musoma vijijini cha kujichukulia sheria mikononi na kuwachomea wenzao nyumba na mali zao baada ya kuwatuhumu kuwa ni wachawi.

Kwa siku mbili mfululizo kati ya Januari 5 na 6 mwaka huu wananchi wa kijiji hicho cha Mwibagi wamechomea nyumba na mali mbalimbali ikiwamo mifugo na vyakula kaya 16 za kijiji hicho wakizituhumu kujihusisha na vitendo vya kishirikina walivyovielezea kuvuruga amani na usalama wa kijiji hicho.

Hata hivyo baada ya serikali ngazi ya wilaya kupata taarifa za uwepo wa tukio hilo iliingilia kati kwa kutuma jeshi la polisi kijijini hapo kuzima tukio huku mkuu wa wilaya hiyo kapteni mtaafu Geoffrey Ngatuni kupitia mkutano wa hadhara kuwataka wakazi hao kutojichukulia sheria mikononi na badala yake waviachie vyombo vya dola vifanye kazi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ambayo imetolewa na kituo hicho,imesema kitendo cha wananchi hao kuwachomea wenzao nyumba na mali zao vikiwamo vyakula ni moja ya vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinavyotakiwa kudhibitiwa kikamilifu na serikali ili visihatarishe hali ya amani na utulivu nchini.

Kupitia tamko hilo CARH inasema kama kulikuwa na tuhuma zozote za kishirikina au za ujambazi dhidi ya watu hao wananchi hao wangetumia taratibu za kisheria ambazo ni kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,

-BUNDA
SERIKALI imesema haitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria watu ambao kwa maslahi yao binafsi watapotosha ukweli halisi wa mchakato wa uundwaji wa katiba mpya unaotarajia kufanywa baadaye mwaka huu.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na waziri wa nchi ofisi ya rais Mahusiano na Uratibu Mh Stephen wasira,wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo maalum la kuhamsisha wananchi juu ya uundaji wa katiba mpya.

Amesema kwa kuwa serikali kupitia vyombo vyake vyote likiwamo bunge la jamhuri imeridhia juu ya uanzishwaji wa katiba hiyo mpya baada ya kusikia kilio cha watu wake juu ya jambo hilo kamwe haitosita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu atakayeonekana kuvuruga mchakato huo.

Mh Wasira ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bunda,ametoa kauli hiyo kufuatia baadhi ya hoja zilizotolewa na wachangiaji katika mkutano huo ambazo amezielezea kama zinalenga kupotosha ukweli halisi wa mchakato mzima wa zoezi hilo.

Hata hivyo mmoja wa wachangiaji katika mkutano huo Bw Frank Kubwera,amesema kuwa katika sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2001 kipo kipengele kinachozuia wananchi kutoa maoni yao juu ya katiba kwenye hadhara yoyote ile na kwamba atakayekiuka hilo atahukumiwa ama kutozwa faini au kwenda jela miaka mitatu au saba na kuomba kiondolewe ili kuwapa watu uhuru wa kutoa maoni juu ya katiba yao.

Hivyo Mh Wasira,amewataka wananchi kote nchini kutoogopa kutoa maoni yao juu ya katiba wanayoitaka kwa makuzi ya amani na utulivu nchini pindi mchakato wa ukusanyaji maoni yao utakapoanza akiwatahadharisha kutumia busara na umakini mkubwa katika hilo kwani bila katiba makini hakuna 
 maendeleo.


,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

-MUSOMA
SERIKALI mkoani Mara,imesema kuwa pamoja na idadi kubwa ya watazania kutegemea kilimo katika kujikombo kiuchumi  na kuchangia uchumi wa nchi lakini kutokuwa na uwezo wa kumudu ununuzi wa zana za kisasa za kilimo kumechangia kudhotesha sekta hiyo.

Kutokana na hali hiyo imewafanya wananchi kulima kilimo cha kujimu tu kwaajili ya kukabiliana na njaa badala ya kilimo cha biashara,hivyo kuwafanya kuendelea kuwa na maisha duni kimaisha.
Kauli hiyo imetolewa na kaimu mkuu wa mkoa wa Mara kapteni mstaafu Geofrey Ngatuni,ameyasema hayo wakati akizungumza na wabunge 18 kutoka katika serikali ya Swiden ambao wako nchini kwa lengo la kuangali hali ya maendeleo ya wakulima na ni jinsi gani watanzania wanavyojikita katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema kuwa hali hiyo kwa wakulima inatokana na wakulima walio wengi kuwa na hali duni ya maisha na kwamba hata wale wakulima walio na uwezo wa kulima kilimo cha biashara wamekuwa wakithiriwa na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kukata tamaa ya kuendeleza kilimo
Aidha amesema kuwa serikali katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi imejiwekea malengo ya kuhakikisha inapanda miti isiyopungua milioni  1.5 kwa nchi nzima.
Amesema amesema kuwa zoezi hilo la upandaji wa miti limekuwa likisimamiwa na serikali lakini miti hiyo inakuwa ni mali ya wananchi wenyewe huku akisisitiza mipango ya Serikali ya kutoa elimu kwa wakulima katika kuhakikisha wanalima kilimo cha manufaa na kisichokuwa na uharibifu wa mazingira.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha wataalamu wa maendeleo ya taasisi  VI  agroforest  Bi Lucy Rwegasira,amesema kuwa mwaka huu ni mwaka wa ushirika duniani hivyo ujio wa wabunge hao pia umelenga kuangalia ni jinsi gani Tanzania imejiandaa katika kuadhimisha maadhimisho hayo.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,
MUSOMA

WABUNGE wa nchi ya Sweden,wamesema njia pekee ya kupambana na umasikini pamoja na kuinua uchumi wan chi kuna haja kwa serikali kuongeza juhudi katika utoaji wa elimu ya kilimo bora na mikopo ya zana za kisasa za kilimo kwa wananchi wake.

Kauli hiyo imetolewa na mmoja ya wabunge 18 kutoka nchjni Sweden Bi Berit Hogman,wakati wakiongea na uongozi wa mkoa wa Mara mjini Musoma.

Amesema ili wakulima waweze kulima kwa tija ni lazima serikali ikaweka mikakati thabiti ya kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo pamoja na kuwawezesha wananchi waweze kulima kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia maziwa,mito na maji mvua ya kukinga katika mabwawa.

Kwa upande wake mbunge mwingine kutoka nchini Sweden Bw Johan Lofstrand,amesema kuwa lengo la laziara yao nchini ni kuangalia maendeleo ya wakulima pamoja na kufahamu mikakati ya kuendeleza kilimo kwa miaka ijayo.

Amesema kuwa ziara hiyo italenga kutembelea afrika mashariki yote hususani katika maeneo yanyopakana na ziwa  Victoria na kuongeza kuwa wamefurahishwa na mazingira mazuri lakini asilimia kubwa ya wakulima ni masikini swala ambalo wamesema kuwa watazungumza na serikali ili waweze kubaini kiini cha tatizo.

,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment