MUSOMA
MWANAUME MMOJA AMEUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KATIKA VURUGU ZA WANANCHI ZILIZOTOKEA KWENYE KIJIJI CHA WEGERO, KATA YA BUSWAHILI, MUSOMA VIJIJINI MKOANI MARA, WAKIWATUHUMU POLISI KUMWACHIA MTUHUMIWA WA MAUAJI ALIYEUA MWENZAKE KWA KUMCHOMA KISU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MARA, KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI (ACP), ROBERT BOAZ, AMESEMA KUWA TUKIO HILO LIMETOKEA JANUARY 14 KATIKA KIJIJI CHA WEGERO, NA ALIYEUAWA KWA KUPIGWA RISASI NI MGOYO MGOYO, MKAZI WA KIJIJI HICHO.
KAMANDA BOAZ AMESEMA KUWA MTU HUYO ALIUAWA KWA BAHATI MBAYA BAADA YA ASKARI POLISI KUJIHAMI KUTOKANA NA KUNDI KUBWA LA WANANCHI KUWAVAMIA NA KUANZA KUWASHAMBULIA KWA MAWE NA NDIPO WALIPOFYATUA RISASI HEWANI NA MOJA IKAMPATA MTU HUYO NA KUPOTEZA MAISHA.
AMEONGEZA KUWA VURUGU HIZO ZILIZUKA KJIJIJNI HAPO KUFUATIA KUWEPO UVUMI KWAMBA MWANANCHI MMOJA ANAYESHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA YA MAUAJI YA KUMCHOMA NA KISU MKAZI MMOJA WA KIJIJINI HAPO DESEMBA 26 MWAKA JANA , AMEACHIWA HURU, BAADA YA NDUGU ZAKE KUWAHONGA POLISI.
KAMANDA BOAZ AMESEMA KUWA KUFUATIA UVUMI HUO WANANCHI WA KIJIJI HICHO WALIKWENDA NYUMBANI KWA NDUGU WA MTUHUMIWA HUYO, MATUTU CHACHA NA NYAMHANGA CHACHA, NA KUZIBOMOA NYUMBA ZAO ZIPATAZO 12, PAMOJA NA KUTEKETEZA MAGHALA YA CHAKULA NA MABANDA YA MIFUGO, WAKIWATUHUMU KWAMBA WAO NDIYO WALIOWAHONGA POLISI NA NDUGU YAO KUACHIWA.
AMESEMA KUWA KUTOKANA NA VURUGU HIZO UONGOZI WA WILAYA YA MUSOMA ULIMTUMA OFISA TARAFA KWENDA KATIKA ENEO LA TUKIO, LAKINI ALIPOFIKA KIJIJINI HAPO WANANCHI WALIMFUKUZA NA NDIPO AKALAZIMIKA KUWAFUATA POLISI AMBAPO PIA POLISI WALIPOFIKA KIJIJINI HAPO, WALISHAMBULIWA NA WANANCHI KWA MAWE NA KUSABABISHA GARI MOJA LA POLISI KUVUNJWA TAA NA VIOO NA ASKARI POLISI MMOJA KUJERUHIWA.
KAMANDA BOAZ AMESEMA KUWA POLISI WALILAZIMIKA KUTOKA KATIKA ENEO HILO KUTOKANA NA VURUGU HIZO KUWA KUBWA HUKU WANANCHI WAKIWA NA SILAHA ZA JADI NA KWAMBA PIA WALIWACHUKUA BAADHI YA VIONGOZI WA KIJIJI HICHO NA KUWAPELEKA KATIKA MAHABUSU KWA AJILI YA KUWAONYESHA MTUHUMIWA HUYO ILI WAWEZE KUWAAMBIA WANANCHI HUO NI UZUSHI MTUPU MTUHUMIWA HUYO BADO YUKO NDANI.
AMESEMA KUWA KUTOKANA NA NYUMBA ZA WANANCHI HAO KUBOMOLEWA NA WANANCHI WENYE HASIRA, SASA FAMILIA ZA WATU HAO ZAIDI YA 30, HAZINA MAHALI PA KUISHI AMBAPO PIA AMETOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MIKONI.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
BUNDA
WANANCHI WANAOISHI NA KUPAKANA NA HIFADHI ZA TAIFA WAMETAKIWA KUTOENDESHA SHUGHULI ZOZOTE ZILIZO KINYUME NA SHERIA ZINAZOTAWALA MASUALA YA UHIFADHI NA BADALA YAKE WASHIRIKIANE NA TANAPA KATIKA KUYAHIFADHI MAENEO HAYO NA RASILIMALI.
RAI HIYO ILITOLEWA MWISHONI MWA WIKI NA KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA PETER MUSAMBA KATIKA HAFLA YA KUKABIDHIWA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO ILIYOTEKELEZWA NA MAMLAKA YA HIFADHI ZA TAIFA(TANAPA) WILAYANI HUMO KATIKA MUSIMU WA FEDHA WA MWAKA 2010/11.
MIRADI HIYO ILIYOIGHARIMU MAMLAKA HIYO ZAIDI YA SHILINGI MIL.180 NI VYUMBA VINNE VYA MADARASA KATIKA SHULE YA MSINGI YA KILORERI;BWENI LA WASICHANA NA VITANDA VYAKE KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA HUNYARI NA ZAHANATI MBILI ZA VIJIJI VYA MIHALE NA KUNZUGU.
PETER AMESEMA IPO TABIA KWA BAADHI YA WAKAZI WA MAENEO HAYO KULIONA SUALA LA KUHIFADHI MBUGA ZA TAIFA NA RASILIMALI ZAKE KAMA JUKUMU LILILOKO MIKONONI MWA TANAPA PEKEE HUKU WAO WAKISHIRIKI KATIKA KUZIHUJUMU KWA KUCHOMA MIOTO;KUWINDA BILA VIBALI NA KUINGIZA MIFUGO NDANI YAKE KINYUME CHA UTARATIBU BILA KUJUA KUWA KWA KUFANYA HIVYO KUNAATHIRI PATO LA TAIFA NA MAENDELEO KWA UJUMLA.
MAPEMA AKIKABIDHI MIRADI HIYO MHIFADHI MKUU WA HIFADHI YA SERENGETI(SENAPA) MTANGO MTAHIKO LICHA YA KUWAPONGEZA WAKAZI WA MAENEO HAYO KWA USHIRIKIANO WAO MKUBWA WALIOUONESHA KWA MAMLAKA HIYO KATIKA KUDHIBITI UHALIFU HIFADHINI PIA AMEWATAKA KUENDELEA KUWAFICHUA WAKOROFI WACHACHE WANAOENDELEZA VITENDO HIVYO ILI WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA.
KWA UPANDE WAO WAKAZI WA VIJIJI HIVYO WALIOONESHA FURAHA ZAO KWA MSAADA HUO AMBAPO WALIUNGANA NA KAULI YA MHIFADHI HUYO MKUU WAKIAHIDI KUPAMBANA HATA MWISHO KATIKA KUWAFICHUA NA KUWAFIKISHA KWENYE VYOMBO VYA DOLA WANAOENDESHA UJANGILI HIFADHINI KWANI WANAHUJUMU RASILIMALI ZA TAIFA ILIYO CHANZO KIKUBWA CHA MAPATO NA MAENDELEO YA WATU WAKE.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
RORYA
WANANCHI WA WILAYA YA RORYA MKOANI MARA WAMETOA MWELEKEO WA MAONI YAO KUHUSU KATIBA WANAYOITAKA KWA KUPENDEKEZA KUINGIZWA KWA KIPENGELE KINACHOITAJA LUGHA YA KISWAHILI KAMA LUGHA PEKEE YA TAIFA.
WAKITOA MAONI YAO WAKATI WA MDAHALO WA KUWAJENGEA WANANCHI UFAHAMU JUU YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA ULIOFANYIKA HIVI KARIBUNI KATIKA MJI MDOGO WA SHIRATI WILAYANI HUMO, WANANCHI HAO WAMESEMA ENDAPO KATIBA HIYO ITAKUWA NA KIPENGELE HICHO MBALI NA KUSAIDIA KUISISITIZA LUGHA HIYO NCHINI LAKINI PIA ITASAIDIA KULITAMBULISHA RASMI TAIFA KUPITIA LUGHA.
WAMESEMA KUTOKANA NA KUTOKUWEPO KWA KIPENGELE HICHO LUGHA HIYO IMEKUWA HAIPATIWI MSUKUMO MKUBWA WA KUFUNDISHWA MASHULENI WALA KUTUMIWA KATIKA MIKUTANO NA MIHADHARA MBALIMBALI.
WAMESEMA KUWA BADALA YAKE IMEKUWA IKICHANGANYWA NA LUGHA YA KIINGEREZA JAMBO LILILOCHANGIA KWA KIASI KIKUBWA KUTOKOMAA KWA LUGHA HIYO ILIYOCHANGIA KWA KIASI KIKUBWA UPATIKANAJI WA UHURU WA TAIFA LETU.
HATA HIVYO WANANCHI WAO WMESEMA PAMOJA NA KUKITAMBUA KISWAHILI KAMA LUGHA YA TAIFA LAKINI PIA MSISITIZO UWEPO KATIKA KUIFUNDISHA LUGHA YA KIINGEREZA MASHULENI HASA SHULE ZA MSINGI ILI KUWAWEZESHA WAHITIMU WA ELIMU HIYO KUMUDU AJIRA KUTOKA KWA WAWEKEZAJI WANAOKUJA NCHINI WASIOJUA VEMA LUGJHA YA KISWAHILI BADALA YA NAFASI HIZO KUISHIA MIKONONI MWA WATU KUTOKA NJE.
MAPEMA KATIKA MAELEZO YAKE MWANASHERIA WA KUJITEGEMEA BONNY MATTO AMESEMA INGAWA TAIFA LINAKITAJA KISWAHILI KAMA LUGHA YA TAIFA LAKINI KATIBA HAIKITAMBUI KWANI HAKIMO NDANI YAKE NA KUWAACHIA WASHIRIKI WA MDAHALO HUO WAAMUE JUU YA JAMBO HILO KAMA WAONA VEMA ITAMBULIKE KIKATIBA AU LA LAKINI AKISISITIZIA KUWA KILA WATAKALOLISEMA LIWEKE MBELE MASLAHI YA TAIFA.
AWALI AKIONGEA KATIKA MDAHALO HUO MRATIBU WA MTANDAO WA ASASI ZA KIRAIA MKOANI MARA(MDF) ULIOANDAA MDAHALO HUO GEORGE MUYABI PAMOJA NA KUWAPONGEZA WANANCHI HAO KWA MICHANGO YAO MBALIMBALI WALIYOITOA LAKINI PIA ALISEMA MAONI YAO YOTE YATAANDIKWA VIZURI NA KUWASILISHWA SERIKALINI ILI YAFANYIWE KAZI WAKATI WA UUNDAJI WA KATIBA MPYA HUKU YAKICHAPISHWA PIA KAMA VIPEPERUSHI NA KUSAMBAZWA KWA WAKAZI WA WILAYA HIYO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment