Rais wa zamani wa Misri Bw Hosni Mubarak amepokea barua yenye tarehe ya kesi yake siku tatu kabla ya kusomewa mashtaka.
Bw Mubarak ambaye amelazwa tangu mwezi Aprili amesaini barua hiyo baada ya kushauriwa na mwanasheria wake, mwanzoni alikataa kusaini barua hiyo.
Ofisa wa hospitali amesema Bw Mubarak aliambatana na mkewe bibi Suzanne na mjukuu wake Omar.
Ofisa huyo amesema hali ya kiafya ya Bw Mubarak inaimarika lakini hali yake kisaikolojia inazidi kuwa mbaya. Bw Mubarak na wanawe Alaa na Gamal, mfanyabiashara Hussien Salem pamoja na waziri wa mambo ya ndani wa zamani watasomewa mashtaka tarehe 3 katika chuo cha polisi.
Habari nyingine zinasema Jeshi la Misri limeondoa mahema ya waandamanaji katika uwanja wa Tahrir yaliyowekwa kusubiria hukumu juu ya Bw Mubarak.
Jeshi limewataka watu wote walioanza kukaa kwenye uwanja huo tangu tarehe 8 Julai waondoke ili kuruhusu watu na magari yapite.
Askari walifyatua risasi kuwatawanya watu hao, na wao walijibu kwa kurusha mawe na kukaidi amri ya jeshi.
SOURCE CRI
No comments:
Post a Comment