Tuesday, August 2, 2011

GRUMETI YAONGOZA KWA KUWA NA KESI NYINGI BARAZA LA USULUHISHI MKOA,

Serengeti,

LICHA ya hoteli ya Sasakwa iliyoko chini ya kampuni ya Singita Grumeti kupata cheti cha hoteli bora ,imebainika kuwa ni miongoni mwa kampuni zenye mashauri mengi ya malalamiko yanayoendelea katika ofisi ya usuluhishi na uamzi ya mkoa wa Mara zilizowasilishwa na wafanya kazi
wa kampuni hiyo.

Katibu wa Chodawu mkoa wa Mara Daudi Mapuga alibainisha hayo wakati
akiongea na Mwananchi kuhusiana na haki za watumishi.

Alisema hiyo inaashiria kuwa viongozi wengi wa kampuni hiyo wanatumia
vibaya nafasi zao,kutokuwatendea haki wafanyakazi na kuibua malalamiko mengi kwenye ofisi za usuluhishi.

"Matumizi mabaya ya nafasi ndiyo chanzo ,kufukuza wafanyakazi bila kuzingatia sheria,makosa madogo yanayohitaji onyo ama kuhojiana yanapelekea kufukuzwa,wengi wanashinda zaidi kupitia mahakamani,hilo ni hatari zaidi kiutendaji,"alisema.

Alisema Chama cha wafanyakazi wa mahoteli,wahifadhi na wanaofanya kazi majumbani(Chodawu)kinawataka viongozi wa kampuni hiyo kutumia zaidi meza ya majadiliano kushughulikia matatizo ya wafanyakazi  kuliko
kufukuza kwa kuwa matokeo yake ni ajira mpya kila wakati.

"Kama chama mkoa tumekubaliana kutoa elimu kwa viongozi wa kampuni na wafanya kazi ili kuhakikisha hayo yanayoendelea na kuiweka kampuni kwenye sura isiyo nzuri yapungue,na wafanyakazi waweze kutimiza wajibu
wao bila misuguano kama inavyojionyesha,"alisema.

Katibu huyo alisema ofisi yake inafuatilia tukio la kupigwa kwa mfanyakazi wa hoteli hiyo Nyangi Kongera(29)na mfanyakazi mwenzake Nikola Bidern raia wa Afrika Kusini na kumfungia kwenye chumba cha baridi,ili haki iweze kutendeka kwa kuwa kumejengeka tabia ya wafanyakazi wa kigeni kuwanyanyasa wazawa na viongozi wa kampunihusika wasichukue hatua.

"Mbali na kupigwa pia tunafuatilia iweje majeruhi ambaye nimlalamikaji kukamatwa na kupelekwa hospitali chini ya polisi ,nakulazimishwa kutoa maelezo ya ugonjwa wake kwa daktari mbele ya polisi watatu,wakati ugonjwa ni siri mgonjwa na daktari,hii haikubaliki na kuna mazingira ya harufu ya rushwa ya kutaka kupoteza haki ya mfanyakazi huyu,lazima tufuatilie mpaka mwisho kulinda haki zake,"alisema.

Alikwenda mbali zaidi na kudai licha ya kutendewa hivyo ,bado jalada
lake lililokuwa na taarifa za vipimo vya madaktari limeibiwa ,"dhamira ya kumtisha na kumtaka atoe maelezo ya ugonjwa  chini ya polisi,nahatimaye kuibiwa kuna mchezo mchafu uliofanywa na viongozi wa hospitali ya Nyerere ddh,hii ni hatari kubwa kwa kuwa anakosa hudumaza matibabu wakati ana madhara"alisema.

Alidai kuwa walifuatilia hata jalada la mwezi februari alilofanyiwa upasuaji wakati anajifungua,nalo limepotea na wamelazimika kufungua jalada la tatu ,hali hiyo pekee inatoa picha kuwa kuna mtandao mkubwa wa kmhujumu mfanyakazi huyo ambaye kwa sasa anaendelea na matibabu,na kuwa suala hilo watahakikisha linapata ufumbuzi hasa waliohusika na hujuma hiyo wawajibishwe.

"Nimeongea na uongozi wa hospitali teule ya Nyerere ddh watoe taarifa iweje majalada hayo yapotee ,huyu hali bado ni mbaya anakosa imani na hospitali hiyo kwa kuwa tayari madaktari na wauguzi wanatumiwa kutaka kupoteza ushahidiwa vipimo,hawajanipa majibu lakini naamini watatoa maana hii ni haki ya mgonjwa kupewa taarifa ya nini kilibainika kufuatia vipimo vyake,'alisema Mapuga.

Wakati huo huo Nyangi ambaye bado analalamika kusikia maumivu makali tumboni hasa sehemu aliyofanyiwa upasuajiambayo anadai alisukumwa na kuangukia makreti ya soda ,amehamishwa katika hospitali ya Nyerere ddh
ambako kumeonekana kuwa na mizengwe mingi ya kumtibu na kupelekwa mjini Musoma kwa ajili ya matibabu zaidi.

Habari zilizothibitishwa na baadhi ya madaktari wa hospitali ya Nyerere kuondolewa kwa mgonjwa huyo,huku ndugu zake wakiwa hawako tayari kuzungumzia uamzi huo kwa sasa kwa madai wanashughulikia mgonjwa mengine watasema.

No comments:

Post a Comment