Sunday, July 31, 2011

YASEMEKANA VIONGOZI NDIYO CHANZO CHA RUSHWA NCHINI

Musoma
 
VIONGOZI wa dini mkoani Mara,wamedai kuwa serikali ndiyo chanzo cha kuchangia kuendelea kwa vitendo vya rushwa nchini kwa kushindwa kuwabana wawekezaji kwa kufuta taratibu na sheria maslahi binafsi ya viongizi.
 
Kauli hiyo ya viongozi hao wa dini,ilitolewa katika warsha ya kujadili mkakati wa kupambana na rushwa ambayo imeandaliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa nchini TAKUKURU mkoa wa Mara.
 
Baadhi ya viongozi hao wa dini Bw Redslaus Manyama ambaye ni mwenyekiti wa baraza la walei kanisa katoliki jimbo la Musoma,alisema serikali ndio chanzo cha rushwa kutokana na kuingia mikataba mibovu isiyo na maslahi ya taifa.
 
“Sisi tunasema serikali ndio inayokumbatia rushwa,kwani imekuwa ikitumia watendaji wake kuingia mikataba mibovu na kuleta wawekezaji wasio na uwezo sasa hayo yote yanafanyika kwa misingi ya rushwa”alisema Manyama.
Naye  mchungaji Okothi Yoga kutoka kanisa la Anglikan dayosisi ya Mara,alidai kuwa hivi sasa viongozi wa serikali na kisiasa wameshindwa kutambua kuwa ni dhambi kubwa kwa mungu na kwa kufanya ni sehemu ya maisha yao ya kila siku.
 
“Serikali inakemea dawa za lakini serikali hiyo hiyo ni chanzo cha kuuzwa kwa dawa za kulevya kwani haiwezekani dawa zikapita mipakana bila rushwa”alisema Yoga.
 
Kwa upande wake katibu wa baraza la waisalam mkoa wa Mara Abdalah Biseko,alimesema ili kukomesha rushwa lazima viongozi wa serikali na watendaji wake wakajitathimini upya katika mapambano dhidi ya rushwa.
 
Naye naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mara  Yustina Chagaka,amesema warsha hiyo inalenga kuwajengea uwezo viongozi wa dini katika kutumia dhamana yao katika jamii kupambana na vitendo vya rushwa.
Mwisho

No comments:

Post a Comment