Sunday, July 31, 2011

DIWANI AAHIDI MAKUBWA KUHUSU MICHEZO BAADA YA KUCHAGULIWA KUONGOZA CHAMA CHA MPIRA

CHAMA cha mpira wa miguu wilayani Serengeti mkoa wa Mara(SEFA)kimepata
viongozi wake baada ya kufanya uchaguzi kwa mjibu wa katiba yao.

Uchaguzi huo uliofanyika jana kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya
hiyo ulitanguliwa na taarifa ya chama ambayo ilionekana kuwa na
mapungufu makubwa ,kutokana na viongozi waliokuwepo kutoshirikisha
wajumbe kwa vikao na kuendesha shughuli za mpira kama kampuni binafsi.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi na ambaye ni mwanasheria wa
halmashauri hiyo Tumaini Nyamhokya alimtaja Mwenyekiti alitechaguliwa
kuwa ni Edward Togocho ambaye ni diwani wa kata ya Kisaka (ccm),Makamu
mwenyekiti mwalimu Samweli Shanyangi,katibu mkuu Francis
Magati,msaiidizi wake ni Daniel Solomoni,Mweka hazina mwalimu Rhobi
Rioba,mjumbe wa mkutano mkuu wa mkoa ni Nyaisa Kyariga,na mjumbe mmoja
wa kamati tendaji kuwa ni Wilson Makindi.

Alisema kuwa nafasi mbili za wajumbe wa kamati tendaji hazikupata
wagombea ,huku mjumbe aliyeomba nafasi ya mwakilishi wa vilabu Charles
Nyangi akienguliwa kutokana na kutokuwa na sifa upande wa elimu kama
kanuni za Tff zinavyoelekeza kuwa angalau awe kidato cha nne,na kuwa
ndani ya siku saba watatangaza na kufanya uchaguzi huo.


Aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanaleta mabadiliko ya michezo
wilayani hapo ,na kuwa nafasi hizo wasizikalie kama visiki
visivyotembea ili kuiweka wilayani hiyo kwenye medani za michezo kwa
kuwa ina jina na sifa kubwa.

Naye mwenyekiti alijigamba kuwa kwa kuchaguliwa kwake atahakikisha
vijana wanapata fursa za kucheza ndani na nje ya mkoa huo,na kuwa sifa
hiyo amekuwa nayo toka akiwa Dar es salaam .

"Mimi nina academy yangu Dar,na hapa nyumbani nimeamua kja kufanya
mambo ambayo yatawasaidia vijana,nafasi imempata mhusika na hata kabla
ya kuchaguliwa nilishawasiliana na wadau mbalimbali kama Serengeti
briweries waweze kutudhamini kwa mashindano mbalimbali,naomba sana
mshikamano kila mmoja atende kulinngana na nafasi yake ,majungu,fitina
havitakuwa na nafasi,ili tupate ofisi maana chama hakikuwa na ofisi
hii ni hatari alisema,"alisema.

Hata hivyo baadhi ya wajumbe walitaka kujua ni jinsi gani
atashirikiana nao kutokana na kuwa anadai shughuli zake ziko Dar es
salaam,hata hivyo alidai kuwa kama anavyoweza kumudu kushiriki vikao
vyote vya baraza la madiwani atafanya hivyo.

mwisho

No comments:

Post a Comment