Sunday, July 31, 2011

SERENGETI BINGWA DUME CONDOM CUP TARIME

TIMU ya Seremara ya mjini hapa, ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Dume Condom Cup, baada ya kuilaza timu ya Polisi Tarime na Rorya bao moja kwa sufuri katika mchezo uliochezwa jana katika uwanja wa Sabasaba mjini hapa, mbele ya mkuu wa wilayani hapa, John Henjewele aliyeshuhudia fainali hizo akiwa mgeni rasimi.

Washika randa, Nyundo na misumali [Seremara ] hao walinyakua ubingwa huo baada ya mchezaji wao hatari Festo Devis alipoifungia timu yake hiyo katika kipindi cha kwanza cha mchezo wa dakika 90, alipoumalizia kuingia wavuni baada ya kipa wa timu ya Polisi Kurwa Maumba Tarime na Rorya kuutema mpira wa adhabu.

Mechi hiyo ilichezeshwa na mwamuzi Zakaria Nyamuhanga aliyesaidiwa na waamuzi wa pembeni Sofia Mtongori na Girishon Kuleba tangu kuanzishwa mashindano hayo, Julai 12, mwaka huu yaliyoshirikisha Timu 16 za wilayani Tarime.

Mashindano hayo yalisimamiwa na shirika lisilo la kiserikali  la nchini hapa la TMARC linalopambana na ugonjwa wa ukimwi nchini  ya msaada wa ufadhili wa Marekani ikiwa lengo kuu ni kuendesha kampeni dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa Ukimwi, kwa kujikinga na mipira ya kiume na kike wakati wa kujamiana mwanamume na mwanamke.

Baada ya mpira huo kumalizika , mkuu wa wilayani hapa, John Henjewele aliwagawia washindi wa mashindano hayo zawadi mbali mbali zilizotolewa na shirika hilo uwanjani hapo.

Mshindi wa kwanza Timu ya Seremara, walikabidhiwa kitita cha pesa tasilimu milioni moja wakati msindi wa pilia Timu ya Polisi Tarime na Rorya walijinyakulia pesa shilingi 750, 000 na mshindi wa tatu Timu ya Supersport walipatiwa shilingi laki tano.

Zawadi zingine zilizotolewa mbele ya viongozi wa chama cha mpira [TAFA] walioshiriki kusaidia kufanikiwa kuendesha mashindano hayo ni pamoja mzee Hadson Manyinyi aliyejinyakulia zawadi ya T shati, kofia na Jezi ya mshabiki bora.

Wengine waliopata furaha uwanjani hapo siku ya jana ni pamoja na kipa wa Timu ya Polisi Tarime na Rorya, Kurwa Baumba aliyapata zawadi ya uchezaji bora , baada ya kuonesha nidhamu na kujituma tangu mashindano hayo kuanza., kwa kupatiwa shilingi laki moja pesa tasilimu.

Ama zawadi nyingine ilikwenda kwa mshindi wa mfungaji bora katika ligi hiyo Edwin Ma Makeka wa Timu ya Seremara aliyejinyakulia  kitita cha shilingi laki moja pesa ya kitanzania kwa sifa ya kuongoza mashindano hayo kufunga magoli mengi zaidi kuliko wengine. 

Katika hatua nyingine katika mchezo huo wa jana, Mchezaji wa Timu ya Polisi Tarime na Rorya ambaye jina lake halikupatika kwa haraka ambaye ni Askari Polisi, alimpiga mwamuzi wa pembeni Girishon Kuleba kwa kumkata ngwala na ngumi,baada ya kuonesha faulo yake ya kuotea wakati mchezaji huyo akielekea kufunga goli eneo la penalti la Timu ya Seremara.

Kwa hatua hiyo mshika kibendera huyo alipatwa na wakati mgumu alipojikuta akifuatwa na kushushiwa  kwqa haraka mapigo hayo kabla ya kuamuliwa vurugu hiyo, alipodaiwa na wachezaji wa Timu ya Polisi Tarime na Rorya kuwa anawapendelea wachezaji wa Timu ya Seremara kwa kuwa ni Timu ya uraini washinde mashindano hayo.

Vurugu hizo zilifanyika kipindi cha Pili mara baada ya mgeni Rasimi mkuu huyo wa wilaya kuwasili mapema mwa mashindano hayo na kukagua timu zote ambapo hatua za dhalula za kutuliza zilifatiwa baada ya Polisi chini ya mwakilishi wa mkuu wa wa Polisi Tarime na Rorya Zakaria .

Hali hiyo ilijitokeza baada ya mchezaji huyo akiwa ndani ya 18 aliotea mapema kabla ya kuvutwa jezi yake na mlinzi mmoja wa Timu ya Seremara alipooneshewa kibendera na mwamuzi huyo wa pembeni na kisha mwamuzi wa uwanjani Zakaria Nyamuhanga kupuliza kipenga, akiwa amechelewa kuona tukio la kwanza la kuotea mchezaji huyo.

Vurugu hizo zilipelekea mchezo huo kusimamishwa kwa muda kadhaa ni kuendelea baada ya kushauliana na kukubaliana na kutolewa kwa adhabu ya kuotea uliopigwa  kuelekea Timu ya Polisi Tarime na Rorya, wakati huo mchezaji huyo wa Polisi Tarime na Rorya aliondolewa kwa kadi nyekundu na kutoka ndani ya mchezo huo.

Mbali ya mchezaji wa Timu hiyo kuondolewa mchezoni pia Timu ya Seremara ilijikuta akitolewa nje ya mchezo huo uwanjani hapo mchezaji wao baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa Timu ya Polisi Tarime na Rorya na kubakia wachezaji wa timu zote mbili kumalizia mchezo wakiwa 10.

Kwa upande wake mratibu wa mashindano hayo na Kiongozi wa Timu ya TMARC Zuberi Mabihe alifurahishwa na wananchi wa Tarime na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kuliko sehamu zingine tangu kuanze ligi ya mashindano hayo na kwamba kwa kupitia mashindano hayo wananchi walijitokeza kwa wingi kupata semina hiyo ikiwa ni pamoja kuchukua mipira ya kiume na kike na kuzifahamu njia ya kujikinga na ukimwi .

Mabihe aliweka wazi kuwa tayari anaamini wananchi hao licha ya kuchukua mipira hiyo,pia walifanikiwa kuelewa njia zingine za kuwa waminifu na mpenzi mmoja na kuvuta subira kabla ya kuolewa na kuoa.

No comments:

Post a Comment