Rorya
UMOJA wa wakulima wa vijiji sita UMONI wilayani Rorya mkoani Mara,umepata hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 40 kutokana na mgogoro ambao umeukumba umoja huo kwa zaidi ya miaka saba hivyo kushindwa kuendeleza shamba la mifugo la Utegi lilonunuliwa na vijiji hivyo kutoka serikalini.
Mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya UDAFCO inayomilikiwa na umoja huo kama kampuni ya kibiahara Otieno Igogo,alisema hayo katika mkutano mkuu maalum wa uchaguzi ambao umetishwa na wanachama kuchagua viongozi wapya kwaajili ya kuendeleza shamba hilo.
Alisema baada ya kununua shamba hilo kutoka tume ya rais ya kubinafsisha mashirika ya umma PSRS mwaka 2004,baadhi ya wanachama waanzisha migogoro kwa kuingiza siasa huku wakipeleka viongozi halali mahakamani hatua ambayo ilisababisha shughuli za umoja huo kusimama kwa kipindi cha zaidi ya miaka saba huku mali ya umoja zikitumiwa bia ya utaratibu.
Hata hivyo Igogo,alisema mgogoro huo ambao ulisababisha kufunguliwa kwa kesi mahakani umedhototesha maendeleo ya UMONI hata kuwafanya wananchi wa vijiji hivyo sita kushindwa kutumia matrekta yaliyonunuliwa kwaajili ya kilimo kushindwa kufanya kazi.
Alisema baada ya kupatikana kwa uongozi mpya kampuni hiyo itatumia taasisi za fedha ikiwemo Benki ya TIB kufufua kiwanda cha maziwa ili kiweze kuzalisha maziwa kwa wingi yakiwemo ya unga baada ya kufungwa mitambo ya kisasa.
Alisema miradi mingingine inayokusudiwa kutekelezwa katika kipindi kifupi ni kuanza kutumia ng’ombe wa umoja huo kuwakopesha wanachama ili waweze kufunga kisasa na kuzalisha maziwa kwa wingi,kuanzisha mradi wa kunenepesha ng’ombe wa nyama na kilimo cha umwagiliaji hatua ambayo itawezesha kuinua uchumi wa wanachama na wananchi wa vijiji hivyo.
Hata hivyo katika mkutano huo,wanachama kwa kauli moja waliwataka baadhi ya viongozi kwa amri ya mahakama kuwatambua viongozi waliochaguliwa ili kuendeleza umoja huo badala ya kuendeleza migogoro ambayo imechangia kukwamisha mipango yao.
Viongozi waliondolewa kwa mujibu wa katiba kwa kushindwa kuitisha vikao kwa kipindi cha miaka saba na kuwafanya wanachama kujiorodhesha kwa mujibu wa katiba na kutoa muda wa kuitisha mkutano mkuu wa uchaguzi ni pamoja na Johanes Igogo,Abdiel Abayo, Sospeter Ombura na Maricus Wakenya wanaodaiwa kuwa na nafasi mbalimbali katika UMONI na bodi ya uendeshaji wa umoja huo.
Katika mkutano huo mkuu maalum ambao umewaondoa madarakani viongozi hao wa zamani kwa kutumia katiba,umewachagua mwenyekiti Gershon Kimori,makamu mwenyekiti Willian Ragoti,katibu Yusuf Otuoma na mweka hazina Albert Wasayi pamoja na wajumbe wa bodi wawili wawili kutoka kila kijiji kuendesha umoja huo kwa kipindi cha miaka mitatu.
mwisho
No comments:
Post a Comment