Umoja wa Afrika umeitaka jamii ya kimataifa kuisaidia Somalia ambayo inasumbuliwa na janga la ukame kwa kiasi kikubwa,huku ikitaarifiwa kuwa takriban watu milioni tatu waishio nchini Somalia wanahitaji msaada wa huduma za kibinaadam.
Mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika Jean Ping amewataka nchi wanachama wa AU kuchangia chochote wawezacho ili kuokoa mamilioni ya raia wa somalia.
Hapo jana Ping alielekeza majeshi ya umoja wa Afrika, AMISOM nchini Somalia kusaidia katika maswala ya usalama mjini Mogadishu ili kuratibu taratibu za upatikanaji wa chakula na huduma nyingine kwa raia.
Source RFI

No comments:
Post a Comment