Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali iliyotolewa muda mrefu kidogo uliyopita, mbio za Mwenge wa Uhuru zitaanza kijijini Butiama tarehe 14 Oktoba mwaka huu, na kumalizika Dar es Salaam. Tarehe 14 Oktoba ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Nyerere, siku aliyofariki Mwalimu Nyerere mwaka 1999.
Dk. Nassoro Matuzya, kiongozi wa mbio za mwenge 2010 akipandisha Mwenge wa Uhuru eneo la Mwitongo wakati wa mbio za mwenge mwaka jana. |
Vyanzo vyangu vya habari vinaniambia kuwa awali sherehe hizi zilikuwa zifanyike Mbeya na pesa za maandalizi zilishatumwa huko. Baada ya uamuzi wa kuhamishia sherehe kuja Butiama taarifa zinaeleza kuwa pesa zilizokwishatumwa Mbeya hazikuweza kupatikana kwa sababu, kwa mujibu wa Serikali mkoani Mbeya, pesa hizo tayari zilikuwa zimeshatumika kwa maandalizi. Hii imeilazimu Serikali kutafuta upya pesa za kugharamia sherehe za Butiama.
No comments:
Post a Comment