Saturday, July 16, 2011

DIWANI TARIME AUWAWA KWA RISASI

DIWANI wa kata ya susuni Felix Holombe (51) ameuwawa kwa kupigwa risasi hadi kufa na watu wasiojulikana  wilayani Tarime mkoa wa Mara usiku wa kuamkia jana.

" Inaonekana alipigwa risasi jana kati ya saa 2 na saa 3 usiku akitoka katika kijiji cha Kiongera akielekea Tarime mjini akiwa na Pikipiki yake" alsema RPC Deus Kato jana asubuhi.

Baada ya watu hao kufanya mauaji hayo waliutelekeza mwili wa marehemu huku wakipora bastora moja ambayo namba zake hazijafahamika, simu mbili na pesa ambazo pia hazijakufahamika haraka.

" Mwili wake umepatikana leo asubuhi katika eneo la Magena na umechukuliwa na kuhifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Tarime" alisema kamanda wa kanda maalumu RPC Deus Kato jana asubuhi.

kwa nujibu wa kamanda Kato  mpaka sasa wauaji hawajatiwa mikononi mwa jeshi la polisi na msako mkali unaendelea .

" Waliofanya tukio hili bado hatujawakamata, tunaendelea kuwatafufuta ili kuwatia mikanoni mwa jeshi la polisi" alieleza RPC Kato

Hiki kilikuwa ni  kipindi cha pili cha uongozi wa Felix kuongoza  kata hiyo ya susuni.

Hata hivyo mauaji ya raia katika wilaya ya Tarime yameendelea kuongezeka japo serikali inaweka ulinzi kwa raia wake.

Hivi juzi mauaji ya ajabu yalitokea katika mji mdogo wa Sirari ambapo Juma Waisiko alikatwa katwa mapanga kwa kutenganishwa viungo vya mwili  kisha kuwekwa kwenye mfuko wa sandalusi na Moi Matari anayeshikiliwa na polisi kufikishwa mbele ya sheria.

mwisho

No comments:

Post a Comment