Monday, July 18, 2011

REBEKAHA BROOKS AKAMATWA

Aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya magazeti ya News International, Rebekah Brooks amekamatwa na polisi inayochunguza kashfa ya udukuzi wa simu pamoja na hongo iliyoendeshwa na gazeti la News of the World.

Rebecca Brooks
Rebecca Brooks
Bibi huyo mwenye umri wa miaka 43 alikamatwa baada ya kualikwa kwenda kwenye kituo cha polisi mjini London.
Sababu ya kukamatwa kwake imeelezewa kama ni kutokana na kumshuku kupanga njama ya kusikiliza mawasiliano kuhusu kashfa ya udukuzi wa simu pamoja na madai ya kuhusika katika rushwa.

Bi.Brooks alikuwa mhariri wa gazeti la News of the World kati ya mwaka 2000 na 2003, wakati ambapo simu iliyokuwa ya binti aliyeuawa Milly Dowler iliingiliwa.

Mhariri wa BBC wa biashara Robert Peston amesema kuwa duru za kuaminika zimethibitisha kuwa mwanamke aliyekamatwa ni Bi.Brooks, ingawa Scotland Yard imekataa kumtaja mwanamke aliyekamatwa.

Makao makuu ya gazeti
Kashfa ya udukuzi ilianzia hapa
Mwandishi wetu anasema pia kwamba kampuni ya News International haikuwa na habari kuwa Bi Brooks atakamatwa wakati wa kujadili hatua yake ya kujiuzulu siku ya jumanne na jumatano ya wiki iliyopita. Hatimaye alijiuzulu mnamo siku ya Ijumaa.

Msemaji wa Bi.Brooks amesema kuwa polisi ya London ilimfahamisha siku hio ya ijumaa, baada ya hatua ya kujiuzulu kwake kukubaliwa kuwa atakamatwa.

Bi Brooks anatazamiwa kufika mbele ya Kamati ya Bunge inayohusiana na masuala ya vyombo vya habari kujibu masuali ya wabunge juu ya kashfa ya udukuzi.

Source BBC

No comments:

Post a Comment