MWANZA
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI PROFESA MARK MWANDOSYA AMESEMA UJENZI WA MAKAZI UNAOFANYWA KATIKA BAADHI YA MIJI MIKUBWA NA MIDOGO INCHINI HAUZINGATII MIPANGO MIJI HALI INAYOSABABISHA HUDUMA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA KUWA NGUMU.
HAYO AMEYASEMA LEO WAKATI AKIZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KWENYE UWANJA WA NYAMAGANA JIJINI MWANZA.
AMESEMA UJENZI HOLELA UNAOFANYWA KATIKA MAENEO MENGI YA MIJI UNASABABISHA SERIKALI KUTUMIA GHARAMA KUBWA KUFIDIA MALI ILI KUPATA NAFASI YA KUPISHA MIUNDO MBINU.
AIDHA WAZIRI MWANDOSYA AMEZINDUA PIA MRADI WA MABWAWA YA MAJI TAKA ENEO LA BUTUJA AMBAO UMEFADHILIWA NA UMOJA ULAYA (EU), SERIKALI YA UJERUMANI NA JAPAN.
MAADHIMISHO HAYO NI YA 23 NCHINI AMBAPO KITAIFA YANAFANYIKA JIJINI MWANZA NA KAULI MBIU YA MWAKA HUU NI MAJI KWA AJILI YA MIJI NA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALI MBALI MIJINI.
No comments:
Post a Comment