Wednesday, September 1, 2010

RUSHWA YAANZA MUSOMA VIJIJINI

WAKATI kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani zikiendelea nchini, imedaiwa mmoja ya wagombea udiwani katika halmashauri ya Musoma vijijini ametoa hango ya zaidi ya milioni 20 kwa baadhi ya wagombea wa udiwani kwaajili ya mandalizi ya kinyang'anyiro cha Uenyekiti wa halmashauri hiyo.
Habari za uhakika ambazo Taifa Letu imezipata zimemtaja kigogo huo kuwa ni Fedelis Kisuka ambaye amekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa miaka kumi mfululizo.
Hata hivyo Kisuka akiongea kwa njia ya simu jana,alikanusha kutoa fedha hizo kwaajili ya kuhonga wagombea hao na kusema hizo ni habari ambazo amekuwa akizisikia kila mwaka.
"Mimi sijatoa hongo kwa mgombea udiwani mwenzangu yoyote hivi nitoe milioni 2 kwa kila mgombea za nini ingekuwa laki mbili au tatu naweza kumsadia mtu sasa milioni zote hizo za nini..kampeni yangu ni kukubalika sina haja ya kutoa hongo hiyo"alisitiza Kisuka.
"Hayo maneno ni ya wapinzani wangu hata wakati wa kampeni za kura za maoni mh Mkono(mbunge mteule wa musoma vijijini)alikuja katika kata yangu na kusema maneno ya kunitukana ili nisishinde lakini nilishinda..hata nyinyi mliniandika mambo mengi mkinituhumu kwa ufisadi lakini yote hayo si kitu kwangu na nimeshinda na kama kweli napendwa hata uenyekiti pia nitashinda bila ya kutumia mamilioni hayo yote"aliongeza.
Wakati Kisuka ambaye anatetea nafasi yake ya udiwani katika kata ya Kukirango akikanusha kutoa hongo hiyo imedaiwa kuwa jumanne wiki hii alikutana na baadhi ya wagombea hao wa udiwani na kuwapa shilingi milioni mbili mbili ili ziwasadie katika kampeni zao za udiwani.
Imedaiwa kuwa zaidi ya madiwani kumi kati ya 34 walipewa kiasi hicho kila mmoja huku diwani mmoja wa kata mmoja ya Tarafa ya Mkongoro ambaye ni miongoni mwa madiwani kumi na tano waolipita bila kupingwa akipewa shilingi laki tano katika mgao huo.
Mmmoja ya madiwani hao aliliambia Taifa letui kuwa mgao wa fedha hizo ulifanyika eneo la Buhemba,ambapo wagombea wa udiwani sita walifika eneo hilo kwa usafiri wa basi dogo la abiria huku wagombea  wanne wa udiwani wakifika eneo hilo kwa usafiri wa pikipiki.
Kampeni za uenyekiti katika halmashauri za wilaya na Manispaa mkoani Mara zimekuwa zikitumia fedha nyingi huku wagombea wakiwasafirisha madiwani kutoka wilaya mmoja hadi nyingine hadi inapofikia siku ya upigaji wa kura hizo.
Akizungumza na gazeti hili katibu wa CCM Musoma vijijini,Bw Ferouz Bhano,alisema chama chake hakijapata taarifa rasmi kuwepo kwa vitendo bali taarifa hizo alidai zimekuwa zikisikika mitaani.
“Bado kama chama hatujapa taarifa rasmi lakini hata hivyo tumeshawaonya wagombea wote kuacha vitendo hivyo tunachokifanya sasa ni kuhakikisha kwanza tunapata ushindi kwa kata ambazo tunagombea..taarifa hizi nimekuwa nikizisikia mitaani na tukipata rasmi tutachukua hatua kwa wahusika”alisema Bhano
 Mwoshooooooooooooooooooo

No comments:

Post a Comment