CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoa wa Mwanza, kimepokea kwa furaha kubwa taarifa za Tume ya Uchagzi (NEC), juu ya kurudishwa kwa jina la mgombea ubunge wa chama hicho katika Jimbo la Nyamagana Jijini Mwanza.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana katibu wa Chadema mkoani hapa Mwanza Bw Wilson Mushumbusi alisema kuwa maamuzi ya NEC ya kurudishwa kwa jina la mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Nyamagana, Ezekia Dibogo Wenje (32) ili kupambana na Lawrence Masha wa CCM kumepokea kwa furaha kubwa jijini humo.
Wenje aliwekewa pingamizi la Uraia na mgombea wa CCM jimbo hilo Masha, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, na baadaye msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo, Wilson Kabwe kuridhia pingamizi hilo na kumuengua mgombea huyo wa Chadema.
"Tumepokea taarifa sahihi kuwa sasa Wenje ni mgombe halali wa ubunge Nyamagana kwa tiketi ya Chadema sasa tunasema kazi imeanza”alisema Mushumbusi.
Kwa mujibu wa Katibu huyo wa Chadema mkoa wa Mwanza, chama kinaandaa mapokezi makubwa yatakayolitikisa jiji kwa ajili ya mgombea Wenje ambaye hivi sasa yupo Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, alisema hivi sasa Chama mkoni hapa kipo katika mikakati maalumu ya kufuatilia ratiba kutoka kwa Msimamizi, kwani hakukuwa na ratiba hiyo baada ya CCM kuamini kuwa mgombea wao Masha hana mpinzani.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment