Saturday, August 21, 2010

WAPINZANIA WA MKONO WAJITOA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

MSIMAMIZI wa uchaguzi wa jimbo la Musoma vijijini amemtangaza mgombea wa ubunge wa chama cha mapinduzi wa jimbo hilo Nimrod Mkono,kuwa mbunge mteule baada ya wapinzani wake sita kujitoa.
Msimamizi huyo wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Musoma vijijini Dk Karaine Ole Kunei,alisema jana mjini Musoma kuwa Mkono aliweza kutangazwa kuwa mshindi baada ya wagombea sita wa vyama vya upinzani kujitoa kwa sababu mbalimbali.
Alisema miongoni mwa sababu zilizowasilishwa kwake zikiambatana na viapo vyao vya mahakama ni kukosa gharama za uendeshaji wa kampeni na kudai kuwa vyama vyao kushindwa kuwawezesha ili kuweza kuendesha kampeni hizo.
Hata hivyo Dk Kunei amesema kati ya wagombea hao sita mmoja ambaye amemtaja kwa jina la Mwita Machael (TLP)ameondolewa katika orosha ya wagombea kwa kushindwa kutimiza masharti ya wadhamini na fomu zake kukosa picha kama inavyotakiwa na tume ya taifa ya uchaguzi.
Wagombea ambao wamejitoa katika kinyanganyiro hicho kwa kula viapo vya mahakamani ni Nyerembe Nyantura(Jahazi Asilia)Rajab Shaban(CUF)Machael Matoke(Chadema)Majungu Ibrahim(Tadea) na Ally Ibrahim(SAU).
Wakati huo huo,tayari chama cha mapinduzi mkoani Mara kimepata ushindi kwa madiwani 22 ambao wamepitwa bila kupingwa,Musoma vijijini ikiongoza kwa kupata madiwani 15,Serengeti madiwani wanne,Bunda madiwani wawili na Rorya diwani mmoja.
Katika hatua nyingine Chama cha Mapinduzi mkoani Mara,kimewaonya viongozi wake kuacha kukihujumu chama chao kwa kutumia viongozi wa mila kupiga kura za koo katika jimbo la Tarime.
Chama hicho pia kimesema hakitasita kuwafukuza ndani ya chama viongozi wake watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo.
Katibu wa CCM mkoani Mara Bw Ndekubali Ndeng'aso,alisema hayo mjini Tarime wakati akizungumza na wagombea wa udiwani na ubunge wa chama hicho wa majimbo ya Rorya na Tarime.
Alisema kuna taarifa ya kuwepo baadhi ya viongozi wa CCM katika ngazi ya wilaya,mkoa na baadhi ya wagombea walioshindwa katika kura za maoni kuwatumia wazee hao wa jadi kukihujumu chama hicho jambo ambalo alisema kamwe halitavumiliwa ndani ya chama.
"Tumesikia kuna viongozi wenzetu wameanza vikao na viongozi wa mila kukihujuma chama chetu..nawaonya viongozi na wagombea wanatajwa kuhusika na vitendo hivyo sisi tumetuma watu wetu kupeleleza na kutukibaini kuhusika kwao hatutaweza kumvulia mtu wa namna hiyo hata kama akiwa kiongozi mwenye cheo kikubwa"alisema Ndeng'aso.
Alisema CCM inaheshimu sana viongozi wa mila katika kuongoza jamii kulingana na taratibu na si jambo jema viongozi hao wa mila wakatumia heshima hiyo kujiingiza kutafutia wananchi viongozi.
Katibu huyo wa CCM mkoani Mara,aliwakumbusha viongozi wanaodaiwa kufanya vitendo hivyo kukumbuka kuwa Tanzania ni nchi yenye makabila mengi na dini mbalimbali na si jambo la busara kuwagawa wananchi kwa kutumia koo kwani alisema kufanya hivyo pia ni kinyume cha katiba ya nchi.
"Kauli yetu ndani ya CCM ni mafiga matatu yaani diwani wa CCM,mbunge wa CCM na kura kwa mgombea urais wa CCM na tukifanya hivyo tutakuwa tumeweka msingi mzuri wa kuharakisha maendeleo yetu kwa kuwa na sauti ya pamoja..hapa tarime CCM inawanachama wengi kuliko chama chochote cha siasa jambo la msingi ni kuhakikisha kipindi hiki tunashinda kwa kishindo katika kurejesha heshima yetu"alisema.
Alisema mbali na jimbo hilo kuongozwa na upinzani kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita lakini Serikali ya CCM chini ya rais Jakaya Kikwete haikuweza kulibagua kimaendeleo katika nyanja zote na kwamba endapo CCM itaiibuka na ushindi katika uchaguzi wa Oktoba 31 kasi ya maendeleo hayo itaongozwa mara dufu kuliko ilivyo hivi sasa ili wana tarime pia waweze kunufaika na keki ya taifa.
Wagombea wa ubunge jimbo la Tarime kupitia CCM ni Nyambari Nyangwine na jimbo la Rorya ni Lameck Airo.
Katika hatua nyingine mbunge wa jimbo la Musoma vijijini aliyemaliza muda wake Nimrod Mkono,ametangazwa kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada ya kupita bila ya kupingwa.
Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Musoma vijijini Dk Karaine Ole Kunei,aliliambia NIpashe Jumapili kwa njia ya simu kuwa Mkono ameweza kutangazwa kuwa mshindi baada ya wagombea sita wa vyama vya upinzani kujitoa kwa sababu mbalimbali.
Alisema miongoni mwa sababu zilizowasilishwa kwake zikiambatana na viapo vyao vya mahakama ni kukosa gharama za uendeshaji wa kampeni na kudai kuwa vyama vyao kushindwa kuwawezesha ili kuweza kuendesha kampeni hizo.
"Wameleta sababu mbalimbali kuwa baada ya kupanga ratiba walitakiwa kufanya kampeni kwa siku 70 sasa wamesema hawana gharama za kampeni huku wengine wakidai vyama vyao vimewatelekeza kwa kushindwa kuwapa fedha za kampeni.
Hata hivyo Kunei alisema kati ya wagombea hao sita mmoja ambaye alimtaja kwa jina la Mwita Machael (TLP)aliondolewa katika orosha ya wagombea kwa kushindwa kutimiza masharti ya wadhamini na fomu zake kukosa picha kama inavyotakiwa na tume ya taifa ya uchaguzi.
Wagombea ambao wamejitoa katika kinyanganyiro hicho kwa kula viapo vya mahakamani ni Nyerembe Nyantura(Jahazi Asilia)Rajab Shaban(CUF)Machael Matoke(Chadema)Majungu Ibrahim(Tadea) na Ally Ibrahim(SAU).

No comments:

Post a Comment