Wananchi Butiama waua Majambazi 3 kwa kuwachoma moto
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuwawa kwa
kushambuliwa na siraha za jadi ikiwemo rungu,mapanga na mawe baada ya kudaiwa
kufanya uhalifu wa kuwateka wavuvi ndani ya ziwa Victoria na kuwanyang’anya
vifaa vyao vya uvuvi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake,kamanda wa
jeshi la polisi mkoani Mara Philip Karangi alisema tukio hilo lilitokea julai 9
majira ya saa 5 usiku katika kisiwa cha Iriga kilichopo Kijiji cha Busamba Kata
ya Etaro Wilaya ya Butiama.
Posted in:
No comments:
Post a Comment