Tuesday, July 1, 2014

Biashara United Musoma yaibamiza Polisi Veteran Musoma mabao 2-0Na Mwandishi wetu

Timu ya soka ya Biashara United ya mjini Musoma Mkoani Mara inayojiandaa ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya soka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwishoni mwa wiki imewabamizia Timu ya Polisi Veteran ya Mjini Musoma mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini hapa.


Mchezo huo ambao ulikuwa na kila aina ya ufundi kutoka kwa wachezaji wa timu zote kipindi cha kwanza kilimalizika baada ya timu hizo kutosha nguvu ya 0-0 

Katika kipindi cha Pili timu hiyo inayoongozwa na Kocha Mchezaji Aman Richard ilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji ambapo katika safu ya ushambuliaji aliingia Augustine Mgendi mabadiliko ambayo yaliinufaisha timu hiyo ya Biashara United baada ya mchezaji huyo kuifungia timu hiyo mabao hayo mawili.

Akiongea baada ya mchezo huo,Kocha huyo alisema kuwa bado timu hiyo inahitaji kufanya maboresho kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge Mjini Dodoma.

Tumeshinda mchezo wetu lakini bado tuna kazi kubwa maana tunapata nafasi nyingi lakini hatuzitumii ipasavyo,sasa kwa mchezo uliopo mbele yetu lazima tubadilike” alisema Kocha Aman

Katika mchezo huo ambao ulishuhudiwa na baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani hapa ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi August mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment