Thursday, June 19, 2014

Lori lililozidi uzito laharibu daraja linalounganisha Sitakishari Ukonga - Segerea

Kuna lori lililokuwa limebeba kontena limejaribu kupita daraja linalounganisha UKONGA {BANANA)- SEGEREA- KINYEREZI NA MBEZI limeharibika kabisa kwa kutumbukia na lori , kwa sasa foleni ni kubwa magari yote yanarudi, kwa wanaotoka mjini ni vyema kutumia njia ya VINGUNGUTI kwenda KINYEREZI, SEGEREA NA MBEZI,
Daraja limearibika sana.NI VYEMA SHERIA IKACHUKUA MKONDO WAKE, haiingi akili mjinga mmoja kukata mawasilino wa watu wote kwenye njia muhimu kama hii.

Mfumo wa kudhibiti malori ya mizigo ni dhaifu sana nchini, madereva wangepewa route za kupita pale wanapotoa mizigo bandari na wanapoingiza mizigo hapa mjini kutoka mikoani,Bila shaka jamaa wametumia mwanya wa polisi/trafic kutofanya kazi usiku kufanya huu utumbo, hivi kwa nini usiku kwa mji mkubwa kama Dar jeshi la polisi linalala mapema HIVYO?

No comments:

Post a Comment