Tuesday, May 27, 2014

Lukaku apiga ‘Hat-Trick’ Ubelgiji ikishinda 5-1, Januzaj ndani


Kiungo wa Manchester United, Adnan Januzaj ameichezea mechi ya kwanza Ubelgiji Jumatatu usiku ikiibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Luxembourg katika mchezo wa kirafiki ambao mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku alifunga mabao matatu.
Januzaj, mwenye umri wa miaka 19, alichagua kuchezea Ubelgiji mwezi uliopita licha ya kwamba ana asili ya Albania, Kosovo, na haya England.
article-2639887-1E3A7C5F00000578-642_634x403
Lukaku amepiga hat-trick yake ya kwanza akiwa na jezi ya Ubelgiji katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Luxembourg.
Lukaku alifunga bao la kwanza dakika ya tatu, akimalizia pasi ya Marouane Fellaini. Joachim aliisawazishia Luxembourg dakika ya 13, lakini Lukaku akaifungia Ubelgiji bao la pili dakika 10 baadaye.
Nyota wa United, Januzaj alichezea mechi yake ya kwanza kikosi cha Ubelgiji akitokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Marc Wilmots, huku Vincent Kompany na Eden Hazard wakipumzishwa.
article-2639887-1E3ACBBF00000578-939_634x511
Mchezaji wa Man United, Adnan Januzaj aliamua kuchezea Ubelgiji mwezi uliopita
Lukaku, ambaye alikuwa kwa mkopo Everton msimu uliopita, alikamilisha mabao yake matatu kabla ya Nacer Chadli kufunga la nne na Kevin De Bruyne kufunga la tano.

No comments:

Post a Comment