Wednesday, May 28, 2014

Kinana atingisha Endasaki na Katesh wilayani Hanang

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi mjini Endasaki, Hanang, jana, Mei 27, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na njia sahihi ya kutatua kero hizo mkoani Manyara
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakiongozana na Vijana wa Kibarbeig kuingia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ofisi ya CCM Kateshi, jana, Mei 28, 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Ofisi ya CCM Katesh, mkoani Manyara
 Kinana akihutubia kwenye mkutano huo wa Katesh
 Mbunge wa Hanang, Mary Nagu akihutubia kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM jimboni mwake kwenye mkutano huo wa Katesh
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo
 Mkuu wa Wilaya ya Hanang Christina Mndeme akisalimia wananchi kwenye mkutano huo wa Katesh
 Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye na Mbunge wa Hanang Dk. Mary Nagu wakijadili jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Katesh mkoani Manyara, Mei 27, 2014. Sumaye amewahi pia kuwa mbunge wa Hanang.
 Kinana akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Igembesabo iliyoibuka bingwa katika michuano ya Vijana wa jimbo la Hanang, wakati wa mkutano wa Katesh
Kinana na Nagu wakikabidhi mizinga ya nyuki kwa vikundi vya vijana Katesh
 Mwanachama wa Chadema akirudisha kadi yake kwa Kinana alipoamua kuhamia CCM kwenye mkutano wa Katesh
 Kinana akipiga mpira wakati Nagu akisubiri kuudaka, wakati wa ufunguzi mashindano ya vijana Endasaki
Endasaki
Kinana  na Sumaye wakishiriki ujenzi Ofisi ya CCM tawi la Qaroda, Hanang. Picha zote naBashir Nkoromo, CCM Blog 

No comments:

Post a Comment