Friday, May 2, 2014

DC BUNDA AZUA MASHINDANO YA ESTHER BULAYA 2014 KWA SABABU ZA KISIASA


Serikali wilaya ya Bunda Mkoani Mara imesitisha Mashindano ya Esther Bulaya ambayo yamekuwa yakifanyika kila Mwaka wilayani humo kwa kile kinachodaiwa baraza la michezo wilayani humo kutoridhishwa na Mazingira ya uwanja wa Sabasaba unatumika kwa Mashindano hayo.
Mwenyekiti wa Mashindano hayo ya Esther Bulaya Bw Flavian Nyamageko alisema Mashindano hayo yamekuwa yakifanyika katika uwanja huo lakini pia wakishirikisha viongozi wa chama cha Soka wilayani humo lakini leo wanashangazwa na kitendo cha chama hicho cha soka kusitisha Mashindano hayo
Mwenyekiti huyo alisema kuwa alipojaribu kuuliza sababu ya kusitishwa kwa Mashindano hayo  viongozi wa Chama cha Soka wilaya ya Bunda wamemweleza ni agizo kutoka kwa mkuu wa wilaya.

 'Tumekuwa tukifanya haya Mashindano kila mwaka tena kwa ufanisi Mkubwa,juzu tumeanza mashindano baada ya kupewa kibali na Chama cha Soka wilaya lakini tunashangaa leo tunaambia tusifanye Mashindano hayo kwa sababu ambazo hazina msingi"alisema Mwenyekiti huyo
Akieleza sababu ambazo zimeainishwa katika barua hiyo Bw Nyamagelo alisema kuwa zipo sababu tatu ambazo zimeelezwa kuwa ni Mazingira kutokuwa rafiki ya kiuchezaji,Chombo kinachotakiwa kuendesha mashindano hayo ni Chama cha Soka na si mwingine,kutokuwepo kwa usalama wa kutosha kulingana na watu wanaohudhuria.
Kiukweli kwetu sisi tunaona hii ni kupingana na ilani ya chama cha Mapinduzi katika kuendeleza Michezo,aliongeza kuwa huu ni mwaka wa nne katika kuandaa mashindano hayo.
Alipotafutwa  Afisa Michezo wilaya ya Bunda mkoani hapa Bw Amos Mtani alisema  ofisi yake bado haijapokea barua yoyote inayoonyesha kusitishwa kwa Mashindano hayo ingawa nakala ya barua hiyo ambayo waandishi wa habari wameipata wilayani hapa inaonyesha  kueleza kutekeleza agizo la Mkuu wa wilaya hiyo lakini afisa michezo huyo hakufika katika kikao hicho.
Wakiongea kwa jazba na waandishi wa habari baadhi ya wadau wa soka wilayani hapa walisema kuwa ni hatari sana kama suala la kisiasa linaingia katika michezo maana kwa hilo inaonekana ni mambo ya kisiasa.
Bw Marwa Juma ambaye alisema kuwa amekuwa mfuatiliaji wa mashindano hayo tangu yameanza amesikitishwa na kusitishwa kwa Mashindano hayo ya Esther Bulaya  Mwaka 2014 kwa kile kinachodai hali ya kiusalama si nzuri lini fujo ilitokea ? alihoji bw Juma
"Tukiendelea kuchanganya chuki na siasa hatutainua michezo katika wilaya yetu" alisema Bw Marwa

Akiongea kwa njia simu kutoka Dar es Salaam Mbunge wa Viti Maalum Vijana Mkoani Esther Bulaya alisema bado anaendelea kuwasiliana na waratibu wa Michuano hiyo lakini hakuna mtu wa kuweza kuizua kwani hiyo ni sera ya Chama cha Mapinduzi.

"Na mimi nimesikia suala hilo na bado naendelea kuwasiliana na waratibu ingawa sidhani kama kuna mtu anaweza kuzia Mashindano hayo kwani hiyo ni sera ya Chama cha Mapinduzi"Alisema Bulaya
Mashindano ya Esther Bulaya yamekuwa yakifanyika kila mwaka kwa misimu minne Mfululizo kwa kuandaliwa na Mbunge wa viti Maalum kupitia vijana ambapo yamekuwa yakiibua vijana  mbalimbali ambapo mwaka huu yanashirikisha timu 72 na wachezaji 1440  katika vituo vya Bunda,Mgeta na kituo cha Nyamswa

No comments:

Post a Comment