Meneja wa Mgodi wa North Mara kushoto Bw Gary Chapman
TARIME
Kampuni ya
uchimbaji Madini ya African Barrick inayomiliki Mgodi wa North Mara imelipa
kiasi cha Dola laki nane sawa na shilingi Bilioni 1 na milioni mia 300 kwa halmashauri
ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara ikiwa ni tozo ya huduma kwa kipindi cha Mwaka
2002 hadi 2005.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika baraza la Madiwani
wa halmashauri ya wilaya ya Tarime mkoani Mara mbele ya Naibu waziri wa nishati
na Madini Steven Masele.
Bw Masele
alisema kuwa pamoja na kukamilisha kwa Malipo hayo lakini mgodi huo unatakiwa
kukamilisha yale yote ambayo wamekubalina ikiwa ni njia ya kuondoa Malumbano ya
Mara kwa Mara kati Mgodi na viongozi wa halmashauri hiyo.
“Mgodi umeahidi kukamilisha makubaliano yote hivyo tuwe
na uvumilivu katika kukamilisha ahadi hizo”alisema Bw Masele
Baada ya
Makabidhiano hayo Naibu waziri huyo akatoa ushauri kwa viongozi wa halmshauri
hiyo kuhakikisha fedha hizo hazileti malumbano katika halmashauri hiyo bali
zile upendo,amani na Maendeleo
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Tarime Nyambari
nyingwine aliomba kutazamwa kwa wale wanaohitaji kulipwa fidia katika maeneo
yanayozunguka mgodi ikiwa ni njia ya kuondoa Malumbano ya Mara kwa Mara huku Meneja
wa Mgodi wa North Mara Bw Gary Chapman akieleza kutolewa kwa fedha hizo ni
ishara ya Kampuni hiyo kutii sheria lakini pia kuleta Mahusiano mema na Jamii.
Kwa Mujibu wa
Naibu waziri Steven Masele amesema mpaka sasa halmashauri nne hapa nchini
zimelipwa Tozo ya huduma Shilingi Bilioni 8 kutoka katika Makampuni ya Migodi
iliyopo katika halimashauri hizo huku viongozi wa halamshauri ya Tarime
wakiahidi kuelekeza fedha hizo katika Miradi ya Maendeleo.
No comments:
Post a Comment