Saturday, March 15, 2014

waumini wa kanisa la wadventist wasabato mjini musoma waadhimisha siku ya vijana kwa kuchangia damu na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa

Mchunga Yohana
 
Mganga Mkuu Mkoa wa Mara Samson Winani
Tuombe


KANISA la Wadiventist Wasabato muungano wa makanisa ya mjini Musoma umetoa msaada wa kuchangia damu katika hospitali ya mkoa wa Mara ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Vijana wa kisabato ulimwenguni inayokwenda sambamba na  siku ya matendo ya huruma.
Akizungumza kwenye maazimisho hayo mara baada ya ibada maalumu ya kuwaombea wagonjwa na zoezi la uchangiaji wa damu,Mchungaji wa Kanisa hilo Yohana  Kado alisema kutokana na kuguswa na uhitaji wa damu kwa wagonjwa mbalimbali wakiwemo wanaotokana na ajali wameamua kutoa msaada huo ili kuifikia jamii kihuduma.
Alisema siku ya vijana wa kisabato ulimwenguni ambayo huazimishwa kila mwaka  machi 15 licha ya kufanya ibada mbalimbali wamekuwa wakiitumia siku hiyo kufanya huduma za kijamii ikiwemo kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watanzania ambao wamekuwa wakifariki kutokana na ukosefu na upungufu wa damu.
Mchungaji Yohana alisema kutokana na kuguswa na suala la umuhimu wa damu kwa wagonjwa katika kuazimisha siku hiyo suala kuchangia limekuwa ni moja la vippaumbele vya vijana wa kisabato na kudai kila mmoja anapaswa kuguswa na matatizo ya damu kwa wagonjwa na kujitoa kuchangia.
Alisema imeshuhudiwa wagonjwa na watu ambao wamekuwa wakipata ajali wakipoteza maisha kutokana na kupungukiwa damu hivyo ni jambo ambalo linapaswa kuchangiwa kwa umuhimu wake ili kuweza kuokoa maisha ya watu hao.
Yohana alisema licha ya waumini hao kuchangia damu pia wametoa misaada mbalimbali ikiwemo ya kifedha,sabuni,mafuta na matunda katika wodi zote za hospitali ya mkoa wa Mara ikiwa ni kuungana na wamini wa dhehebu hilo ulimwenguni kote katika siku ya vijana na matendo huruma. 
Meneja Mpango wa Damu salama Kanda ya Ziwa docta Fredrick Venance amelishukuru Kanisa la Wadiventist Wasabato mjini Musoma kwa kuguswa na suala la kuchangia damu na kuiomba jamii nyingine kuona umuhimu wa kuchangia ili kuokoa maisha katika jamii.
Alisema katika suala la uchangiaji wa damu bado kuna changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya watu kuona wanaweza kupata maradhi pale wanapochangia damu ama kudhoofika mwili kitu ambacho sio kweli na kumuomba kila mmoja kwa moyo wa huruma kuchangia damu.
Venance alisema waumini hao wamechangia chupa 120 za damu ambazo mara baada ya kufanyiwa uchunguzi wa viwango itaokoa maisha ya watu ambao watafikishwa mahospitalini wakiwa na matatizo ya damu wakiwemo wagonjwa wa kawaida na wale wanaopata ajali.
 
source Binda

No comments:

Post a Comment