WADAU wa soka mkoani Mara wamekitupia lawama chama cha
soka mkoani humo(FAM) kwa kile walichodai kuitengenezea mazingira timu
ya JKT Rwamkoma kuchukua ubingwa ili iuwakilishe mkoa.
Wakizungumza
mara baada ya mchezo ulioipa ushindi wa mabao 12-0 JKT dhidi ya timu ya
Wasaga FC,wadau na mashabiki wa soka walidai tangu mwanzoni mwa
ligi(FAM)wamekuwa wakiitengenezea mazingira timu hiyo kwa kile
walichokidai kuziona timu nyingine haziwezi kusafiri.
Walisema
katika mchezo huo JKT Rwamkoma walikuwa hawana uwezo wa kutoka na
matokeo hayo ya ushindi kutokana na mchezo huo na kuiomba TFF kufatilia
kwa makini na kuomba taarifa ya mchezo kutokana na mazingira hayo
kuzikatisha tamaa timu nyingine kushiriki ligi msimu ujao.
Mmoja
wa dau hao aliyefahamika kwa jina la Philipo Janja alisema kamwe soka
la mkoa wa Mara halitaendelea kutokana na kile alichokieleza viongozi
kuzikumbatia timu ambazo hazina
uwezo na kila msimu mkoa wa Mara wamekuwa wasindikizaji kwenye ligi ya
Taifa.
Akitolea mfano timu ya Baruti FC
iliyomaliza katika nafasi ya pili kwa kuzidiwa na JKT Rwamkoma kutokana
na tofauti ya magori ya kufunga,Janja alisema ilikuwa ni timu yenye
wachezaji waliokaa pamoja kuanzia msimu uliopita na hali ya ushindi wa
mabao 12 wa JKT Rwamkoma aliodai wa kupangwa umewakatisha tamaa.
"Mimi naweza kusema Baruti Fc ilikuwa ni timu bora kwenye haya Mashindano maana hata ukiangalia mechi zao wanacheza kwa malengo,kwa stahili hii itakuwa ngumu"alisema Janja
Alisema
lazima chama cha soka mkoa wa Mara(FAM) ni lazima wabadilike nakuona
kila timu inayoingia kwenye mashindano inao uwezo wa kusafiri na kuacha
kuzibeba timu ambazo wanadhani zinauwezo na matokeo yake zinakuwa
wasindikizaji kwenye ligi ya taifa.
Alipotafutwa
ili kuweza kuzungumzia malalamiko hayo ya wadau na mashabiki wa soka
mkoani Mara,katibu wa (FAM) Mugisha Galibona hakuweza kupatikana
uwanjani wala simu yake ya mkononi huku ikidaiwa alikwenda kutuma jina
la bingwa wa
mkoa TFF kutokana na kuogopa kuchelewa kulituma.
Katika mchezo wa mwisho timu ya Baruti Fc iliibamiza timu ya Musoma Shooting mabao 3-1 huku timu ya JKT Rwamkoma ikiibuka kidedea kwa kuwa bingwa wa mkoa wa Mara 2014 baada ya kuifunga timu ya Wasaga FC mabao 12-0
No comments:
Post a Comment