Monday, March 24, 2014

African Barrick kuanza kuajiri wazawa


TENDAJI MKUU WA KAMPUNI YA AFRICAN BARRICK GOLD MR BRAD GORDON AKIELEZEA SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA MIGODI YA BARRICK NCHINI NA MIKAKATI WALIYONAYO KWA MWAKA 2014.
Kampuni ya African Barrick Gold imesema kuwa kuwa bado inaendelea na mpango wa kuwapunguza waajiriwa wakigeni ili kuzidi kuwapa nafasi watanzania kufanya kazi katika migodi yake kwenye ngazi za juu na kati.
Hayo yameelezwa na mtendaji mkuu wa African Barrick Brad Gordon katika kongamano la wadau wa sekta ya madini kanda ya ziwa lililofanyika katika hotel ya Malaika jijini Mwanza.
Gordon amesema kuwa wakati migodi ya Barrick inanza ilikuwa na wafanyakazi wa kigeni wapatao 421 lakini wamepunguzwa na kufikia 290 sawa na punguzo la asilimia 29.
Ameongeza kuwa kwa mwaka 2014 Kampuni yao ina mapngo wa kuwapunguza zaidi wafanyakazi kutoka nje ya Tanzania licha ya kwamba hakufafanua watawapunguza kwa asiliamia ngapi.
Sambamba na hayo Gordon ameelezea changamoto zinazoikumba migodi yake nchini Tanzania kwamba ni pamoja na kiwango kidogo cha umeme kinachotolewa na Shirika la umeme nchini TANESCO pamoja na uvamizi wa maeneo yao ambayo yana leseni za Barrick unaofanywa na wachimbaji wadogo.
Akiongezea Gordon amesema kuwa changamoto nyingine ni fidia za ardhi ambazo kwa Tanzania ni kubwa sana  pamoja na ukosefu wa wataalamu wa kusimamia shughuli za uchimbaji madini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Mwanza Mh.Antony Dialo ameipongeza kampuni ya African Barrick Gold kwa shughuli zao wanazozifanya katika jamii na amewashauri kutangaza na kuonyesha jamii ili waondokane na dhana kwamba wawekezaji wa sekta ya madini hawana msaada kwa jamii hizo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya ambaye alikuwa mjumbe katika kongamano hilo amewasisitiza ABG kulipa kodi ya huduma wanazodaiwa na Serikali (Service Leavy) ili kuondoa sintofahamu katika Halmashauri na kuwapa nafasi wanasiasa kufanya kama kigezo cha kampeni katika kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
Akijibu suala hilo mtendaji mkuu wa ABG Mr Gordon amesema kuwa suala hilo wamelipokea na kwamba mwishoni wa mwezi wa nne mwaka huu ufumbuzi utakuwa umepatikana.
Akihitimisha kongamano hilo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga amewashukuru ABG kufanya kongamano la wadau wa nishati ya madini kwa mara ya kwanza kanda ya ziwa na kuwataka wazidi kutoa huduma za kijamii katika maeneo ambayo migodi yao inapatikana.

MATUKIO KATIKA PICHA:
MKUU WA MKOA WA MWANZA ENG.EVARIST NDIKILO AKIFUNGUA KONGAMANO HILO.
MWANDISHI WA RADIO FREE AFRICA NA MMILIKI WA BLOG YA KIJUKUU CHA BIBI K WA KWANZA KULIA AKIWA KATIKA KONGAMANO HILO KUHAKIKISHA ANAIJUZA JAMII NINI KINACHOENDELEA KATIKA KONGAMANO HILO LA WADAU WA SEKATA YA MADINI KANDA YA ZIWA.
MENEJA MWANDAMIZI WA KAMPUNI YA AFRICAN BARRICK GOLD BI JANET REUBEN KULIA AKISIKILIZA MAELEZO YA MKUU WA MKOA WA MWANZA MARA BAADA YA KONGAMANO KUFUNGULIWA.

WADAU WA SEKTA YA MADINI KANDA YA ZIWA WAKIWA KATIKA KONGAMANO HILO.

MSIMAMIZI NA MWONGAZAJI WA KONGAMANO HILO AKIENDELEA NA RATIBA.

WADAU TOKA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIZA TRA.

WAANDISHI WA HABARI TOKA VYOMBO MBALIMBALI JIJINI MWANZA WAKIWA KATIKA KONGAMANO HILO.

KUTOKA KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA KAHAMA BENSON MPESYA KATIKATI NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA FELIX KIMARIO NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA TARIME KULIA.

WADAU WAKIWA KATIKA KONGAMANO HILO.

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MWANZA MH.ANTONY DIALO AKITOA USHAURI KWA ABG.

KUTOKA KUSHOTO NI MAKAMU WA RAIS WA AFRICAN BARRICK GOLD MR.DEO MWANYIKA KATIKATI NI MTENDAJI MKUU WA KAMPUNI HIYO GRAD GORDON WAKISIKILIZA MASWALI TOKA KWA WADAU.

MH ANTONY DIALO KUSHOTO KATIKATI NI MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ALLY RUFUNGA NA KULIA NI MKUU WA MKOA WA MARA MH.JOHN TUPPA WAKISIKILIZA KWA MAKINI MIPANGO YA ABG KWA MWAKA 2014.

MKUU WA MKOA WA MARA MH.JOHN TUPA AKIULIZA SWALI NI LINI ABG ITAANZA KUINGIA UNDERGROUND KATIKA MGODI WAKE WA NORTH MARA.

MKURUGENZI WA TARIME AKIULIZA SWALI.

MDAU TOKA HALMASHAURI YA MSALALA AKITOA UZOEFU WAO NAMNA WANAVYOFANYA KAZI NA KAMPUNI YA ABG.

MDAU AKICHANGIA HOJA KATIKA KONGAMANO HILO.

WAANDISHI WA HABARI WAKIFANYA MAHOJIANO NA MAKAMU WA RAIS WA ABG MR.DEO MWANYIKA MARA BAADA YA KUMALIZA KONGAMANO.
 
source william bundala

No comments:

Post a Comment