
Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie Nsoka
akizungumza na wahariri na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
Makao Makuu ya Ofisi hizo, Sinza Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie Nsoka
akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali
vya habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwa katika mkutano huo.

Sehemu
ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali
vya habari nchini wakifuatilia mada katika mkutano huo.

Mmoja wa wahariri kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Lilian Timbuka (wa kwanza kushoto) akichangia mada katika mkutano huo.
MKURUGENZI Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake
(TAMWA), Valerie Nsoka amevipongeza vyombo vya habari kwa kutoa
ushirikiano wa uandishi wa habari za ukatili wa kijinsia ambao umeonesha
mafanikio kwa sasa ukilinganisha na mwamko uliokuwepo miaka ya nyuma.
Bi. Nsoka ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa
akiwasilisha taarifa ya matokeo ya utafiti wa mradi wa GEWE II (Mpango
wa kutokomeza ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na
watoto) kwa wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo
mbalimbali vya habari nchini.
Alisema kwa kipindi cha kuanzia Oktoba 2012 hadi Septemba 2013, jumla
ya habari 499 ziliandikwa kwenye magazeti mbalimbali kupitia mradi wa
GEWE, huku habari 216 zikiandikwa kwenye miradi mingine ya taasisi hiyo
hivyo kufanya idadi ya habari zote kufikia 715 kwa mwaka.
Alisema ongezeko hilo limeleta mafanikio kadhaa kwa jamii hivyo
kuwaomba waandishi wa habari waongeze juhudi za uandishi wa habari za
ukatili wa kijinsia ili kukomesha vitendo hivyo vinavyo endelea
kuiathiri jamii.
“…Hali inaonesha uchapishaji wa habari uliongezeka zaidi kwa vitendo
vya ukatili, ukilinganisha na kipindi cha mwaka 2012 ambapo uchapishaji
wa habari katika magazeti ulikuwa na Idadi ya 350 kwa miradi yote ya
TAMWA,” alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema ongezeko hilo la uandishi wa habari za ukatili wa kijinsia
limeleta mafanikio kwa kiasi fulani, kwani kwa sasa jamii imepata uelewa
kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na waliokuwa wakinyanyasika sasa
wamejitokeza kuomba msaada zaidi.
“…TAMWA imekua ikipokea simu kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania
watu wakiomba msaada wa kutatuliwa matatizo yao. Kituo ha usuluhishi cha
TAMWA kimekua kikipokea watu wakisema wamepata habari baada ya kusoma
au kuona machapisho au tangazo kupitia luninga au kusikiliza redio…,”
alisema Bi. Nsoka.
Aidha alisema waandishi wa habari wa Dar es salaam na mikoa mingi
sasa wameweza kuandika na kutangaza habari mbalimbali za ukatili wa
kijinsia kwa ufasaha.
Akizungumzia matokeo ya utafiti wa kihabari uliofanywa na TAMWA kwa
kushirikiana na waandishi wa habari, alisema utafiti ulibaini kuwa
asiliamia 17 ya wananchi hawana uelewa wa sheria za ukatili wa kijinsia,
huku Mkoa wa Lindi kupitia Wilaya ya Lindi Vijijini ikiongoza kwa
kupata asilimia 12.
Alisema utafiti huo uliowahoji jumla ya watu 2,300 pia ulibaini kuwa
asilimia 47 za kesi huripotiwa katika Serikali za vijiji na asilimia 25
huripotiwa katika vituo vya polisi. Utafiti ulinesha kuwa wananchi
hawana majukwaa ya kukaa pamoja na kujadili changamoto zao ambapo ni
asilimia 13.5 ndiyo wanachama wa asasi za kijamii.
TAMWA kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari kiliwatuma
waandishi wa habari kwenda katika Wilaya 10 za mradi na kufanya utafiti
ambao matokeo yake yalitolewa mwezi Julai 2013. Wilaya 10 za Tanzania
Bara na Visiwani, ni pamoja na Kinondoni, Ilala, Kisarawe, Mvomero,
Ruangwa, Lindi Vijijini, Newala, Wete, Unguja Mjini Magharibi na Unguja
Kusini.
No comments:
Post a Comment