Mkurugenzi Mkuu wa PSPF akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Kalenda ya Mwaka 2014 Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw John G.Tuppa.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF akizungumza na Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa Mkoani Mara katika ukumbi wa uwekezaji Mkoani Mara.
Maafisa wa PSPF
Mjasiriamali Amani Richard akinena jambo
Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw John G. Tuppa akinena Jambo katika chakula cha jioni
Nipe paja hilo
MUSOMA
MFUKO wa Pensheni
kwa Watumishi wa Umma PSPF umetangaza mkakati wa kuwanufaisha
Watanzania ambao si watumishi wa umma kwa kujiunga na mfuko wa uchangiaji kwa hiari wa PSS huku makundi ya Wajasiliamali,Wavuvi,Wakulima
na makundi mengine katika jamii ambayo yamejiajiri katika sekta isiyo rasmi
yakipewa kipaumbele katika mfuko huo.
Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa PSPF Bw Adam Maingu,alitoa kauli hiyo mjini Musoma wakati akizungumza na viongozi,wawakilishi na wanachama
wa mfuko huo katika wilaya ya Musoma na Butiama mkoani Mara.
Alisema kwasasa mfuko huo wa kuchangia kwa hiari utakuwa
ni mkombozi mkubwa kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya watumishi wa Umma,Sekta
binafsi na wafanyabiashara kujiwekea akiba kwa kuchangia kiasi cha kuanzia elfu
kumi na kuendelea.
Kwa upande wake mkuu mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Gabriel
Tuppa,akizungumza katika hafla hiyo,ameupongeza uongozi wa mfuko huo kwa
kukutana na wadau wake kwaajili ya kupata maoni ambayo yatasaidia kuboresha
utendaji wao wa kazi
lakini akiwataka watendaji wa Mfumo huo kujenga imani kwa
wanachama wao endapo watapunguza gharaza za uendeshaji ili gharama zingine
zirudi kwa wanachama
Nao baadhi ya washiriki katika hafla ambayo ni watumishi
wa Serikali na Sekta binafsi wametoa maoni mbalimbali katika kuboresha Mfuko
huo huku wakitaka wanachama kupewa kadi za uanachama
No comments:
Post a Comment