Thursday, February 13, 2014

Makamu wa Rais wa Tanzania afungua Kongamano la siku tatu la uwekezaji lililoandaliwa na Mikoa sita ya Kanda ya Ziwa

MAKAMU wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal amesema kuwa Serikali ya awamu ya nne itaendeela kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini kwa lengo la kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Makamu Rais Dkt Bilal ameyasema hayo jijini Mwanza wakati akifungua kongamano la siku tatu la uwekezaji lililoandaliwa na Mikoa sita ya Kanda ya Ziwa katika Hoteli ya Malaika Beach Resort na kuwashilikisha washiriki zaidi ya 1000 toka ndani na nje ya nchi.
Alisema kuwa Serikali tayari imechukua hatua za makusudi kuboresha mazingira ya Uwekezaji katika kuanzisha na kufungua biashara,kupunguza urasimu wa upatikanaji wa leseni za biashara,uboreshaji wa sheria za mikataba ya kazi.
“Kwa kiwango kikubwa Serikali imedhibiti rushwa na kurekebisha masuala ya ksiera na sheria lengo likiwa ni kuhakikisha inavutia wawekezaji hapa nchini”,alisema Makamu wa Rais Dkt Bilal
.
Dkt Bilal alisema kuwa ili kuwe na uhakika wa masoko kwa bidhaa zinazozalishwa na wawekezaji wa ndani,Serikali imeingia mikataba mbalimbali na maridhiano katika uwekezaji na amsoko ya kimataifa kwa kushirikiana na AGOA,SADC,na COMESA.
Makamu wa Rais aliipongeza Mikoa ya Kanda ya ziwa kutokana na kuamua kufanya Kongamano hilo muhimu kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii pamoja na raslimali zilizopo katika Mikoa ya kanda ya ziwa.
Alisema kuwa mikoa hiyo imebahatika kuwa na idadi kubwa ya watu pamoja na raslimali lukuki ambazo zinahitajika kuendelezwa kwa ajili ya kuongeza pato la taifa.

Source Gsengo
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Everist Ndikilo alisema kuwa wakuu wa mikoa wa Mikoa ya Kanda ya ziwa waliafikiana kufanya kongamano la kuvutia wawekezaji na kueleza kuwa kongamano hilo ni la aina yake kufanyika hapa nchini kwa kuandaliwa na mikoa sita kwa pamoja.

Awali Mwenyekiti wa Kongamano hilo Waziri wa zamani katika Wizara mbalimbali Sir George Kahama,aliitaka Serikali kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya kuunganisha mikoa ya kanda ya ziwa na wawekezaji toka ndani na nje ya nchi.
Sir Kahama alisema kuwa uwanja wa ndege wa Mwanza unapashwa kujengwa kwa kiwango cha kimataifa na kushangazwa na kusua sua kwa ujenzi wake hivyo kuinyima fursa mikoa ya kanda ya ziw akufanya baishara za kimataifa kupitia uwanaj wa ndege wa Mwanza.


No comments:

Post a Comment